Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanal Evans Mtambi amekunatana na kamishina wa Uhamiaji nchini Dkt Anna Makakala ambaye yuko ziara katika Mkoa wa mara .
Akizungumza mara baada ya kuwasili Mkoani mara Kamishina wa uhamiaji Dkt Anna Makakala amempongeza Mkuu wa Mkoa kuaminiwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kumsaidia katika Mkoa huo wa mara.
Pamoja na mambo mengine Kamishina alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa uhamiaji wanaendelea na zoezi la kuandikisha walowezi ambapo wanadai vitambulisho.
Nazaidi ya yote tunaendelea kujipanga kuelekea Uchaguzi mwakani na uchaguzi wa serikali za mitaa tunaendelea na zoezi la kuwandikisha walowezi “Butiama kuna kundi la watu walihamia kutoka Kenya wanadai vitambulisho vya utaifa tunaendelea kulishughulikia Tatizo lao tunapokelekea katika uchaguzi swala kama hilo huwa linajitokeza kwa walowezi nao Kupata vitambulisho vya wapiga kura ili tunapofika au wanaopiga kura wafanye wale wanaopaswa kufanya hivyo”Alisema Dk.Anna Makakala Kamishina wa Uhamiaji Nchini.
Mkuu wa Mkoa wa mara Kanali Evans Mtambi amemuomba Kamishina wa uhamiaji kuliangalia kundi la walowezi kwa jicho la ziada hususani kuelekea katika chaguzi.