Kaimu Naibu Rasi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Coretha Komba (Wapili kutoka kulia) akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya wanaume ya BPA 1 Abdulharizi Saidi baada ya timu hiyo kuibua na ushindi dhidi ya timu ya BPA 3 katika mchezo wa fainali wa mashindano ya madarasa 2024 uliochezwa Julai 6, 2024 katika Viwanja vya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam
Mratibu wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Kituo Cha Tegeta Dkt. Janeth Swai (Watatu kutoka kulia) akimkabidhi Zawadi nahodha wa timu ya mpira wa Pete ya wanawake BPA 1 Luncy Ezekiel baada ya timu hiyo kuibua na ushindi dhidi ya timu ya BPA 3 katika mchezo wa fainali wa mashindano ya madarasa 2024 uliochezwa Julai 6, 2024 katika Viwanja vya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Kituo Cha Tegeta
Mgeni Rasmi wa Mashindano ya Madarasa 2024 Kaimu Naibu Rasi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Coretha Komba akiwa
Mratibu wa Kituo Cha Tegeta Dkt. Janeth Swai, Naibu Mshauri wa Wanafunzi Ndaki ya Dar es Salaam Bi. Zitta Victoria Mnyanyi, Kaimu Mwalimu wa Michezo Ndaki ya Dar es Salaam Bw. Joseph Ally Sule wakikagua timu kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali ya mashindano madarasa 2024.
Wachezaji wa timu ya mpira wa Pete BPA 1 na BPA 3 wakiwa katika mchezo wa fainali ya mashindano ya madarasa 2024 katika Viwanja vya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Kituo Cha Tegeta.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu BPA 1 na BPA 3 wakiwa katika mchezo wa fainali ya mashindano ya madarasa 2024 katika Viwanja vya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Kituo Cha Tegeta.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya BPA 1 wakiwa katika picha ya pamoja.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya BPA 3 wakiwa katika picha ya pamoja.
Mgeni rasmi wa Mashindano ya Madarasa 2024 Kaimu Naibu Rasi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Coretha Komba akizungumza jambo na wanafunzi wa Chuo hicho kabla ya kuanza zoezi la kugawa zawadi kwa washindi.
Mratibu wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Kituo Cha Tegeta Dkt. Janeth Swai akizungumza jambo na wanafunzi wa Chuo hicho kabla ya kuanza zoezi la kugawa zawadi kwa washindi.
Kaimu Mwalimu wa Michezo Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Bw. Joseph Ally Sule akizungumza jambo na wanafunzi wa Chuo hicho kabla ya kuanza fainali za mashindano madarasa 2024.
Naibu Mshauri wa Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumb Ndaki ya Dar es Salaam Bi. Zitta Victoria Mnyanyi akizungumza jambo na wanafunzi wa Chuo hicho kabla ya kuanza fainali za mashindano madarasa 2024.
Picha za matukio mbalimbali
………..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Mashindano ya Madarasa 2024 Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam yamfikia tamati, huku timu ya mpira wa miguu ya wanaume na Pete kwa wanawake ya BPA 1 zimefanikiwa kuchukua Kombe la Mashindano hayo baada ya kupata ushindi katika mchezo wa fainali ya iliyofanyika Julai 6, 2024 katika viwanja vya Chuo Kikuu Mzumbe Kituo cha Tegeta, Dar es Salaam.
Nafasi ya pili kwa mpira wa miguu na Pete imeshikwa na BPA 3 katika mashindano ya madarasa 2024 ambayo yalikuwa na lengo la kuhamasisha michezo kwa ajili ya kujenga afya ya mwili na akili kwa wanafunzi jambo ambalo litasaidia kuwa na afya njema na kushiriki masomo kikamilifu.
Akizungumza wakati kukabidhi zawadi kwa washindi Kaimu Naibu Rasi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Coretha Komba, amesema kuwa ni muhimu wanafunzi kushiriki michezo kwani yanaleta upendo, mshikamano pamoja amani.
Dkt. Komba ambaye ni mgeni rasmi katika fainali za mashindano hayo, amesema kuwa michezo inasaidia kuchechea afya ya akili ambayo inaongeza ufansi katika kufikili vizuri pamoja kutekeleza majukumu ya kila siku.
“Mashindano haya yanasaidia kuibua vipaji vya wanafunzi, naomba tuendelee kufanya mazoezi, Chuo kinaitaji wanafunzi wenye afya njema” amesema Dkt. Komba.
Amefafanua kuwa mwitikio wa ushiriki wa michezo katika Chuo hicho ni mkubwa kwani wanafunzi wengi wamekuwa na hamasa ya kushiriki mashindano hayo na kujiona ni sehemu ya chuo kikuu mzumbe ndaki ya Dar es Salaam.
Kaimu Mwalimu wa Michezo Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Bw. Joseph Ally Sule, amesema kuwa mashindano hayo yalishirikisha wanafunzi wote wa Chuo hicho na kuonesha ushindani mkubwa.
Bw. Sule amesema kuwa kutokana na uhitaji wa ushiriki wa michezo mbalimbali kwa wanafunzi mwaka 2025 wanatarajia kuongeza idadi ya michezo ili kila mwanafunzi apate fursa ya kushiriki.