Wafanyabiashara wametakiwa kutumia fursa zilizopo kati ya Tanzania na Jamhuri Korea ili kufaidika na soko la bidhaa mbalimbali ambazo nchi hizo limeonyesha kuzihitaji zaidi .
Akizungumza jana wenye maonesho ya 48 ya Kibiashara ya Kimataifa ikiwa leo ni siku Maalum ya biashara ya Jamhuri Korea kama sehemu ya mwendelezo wa kutoa fursa kwa mataifa mbalimbali kuonesha biashara zao na tamaduni, Katibu Mkuu wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Fatma Maborok Khamia, amesema lengo kuu siku maalumu ya Jamhuri ya Korea ni kuwakutanisha wafanyabiashara kati ya Tanzania na Korea Kusini.
“Fursa kubwa kushirikiana suala muhimu kuweka export Tanzania na kampuni za Tanzania zina fursa kupeleka bidhaa Jamuhuri ya Korea ikiwemo Korosho karafuu, chai na kahawa,”amesema.
Amesema wameona Kampuni za Tanzania zina fursa ya kujifunza teknolojia ya kisasa kwenye uzalishaji bidhaa wameendelaea kwenye teknolojia.
Fatma ameeleza kuwa wafanyabiashara nchini wanapaswa kujifunza namna gani wameweza kuboresha bidhaa katika teknolojia ya kisasa katika uzalishaji kuboresha thamani ya bidhaa.
Amesema kuwa viongozi wanapaswa kuhamasisha wawekezaji kuwekeza Tanzania watanzania watakiwa kuchangia mkia fursa zinazotengenezwa na viongozi.
Amesema amewasikiliza wafanyabiashara wameeleza changamoto.m wanazokabiliana nazo ambapo yeye na Katibu Mkuu kuto bara watajadiliana kutatua changamoto hizo.
Akizungumza kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Bisahara Tanzania (Tantrade),Meneja wa Masoko wa Ndani na Nje wa Tantrade Dorothy Urio amesema wadau kutoka Korea wanahitaji madini,korosho na mengine kutoka Tanzania hasa kuboreshamnyororo wa thamani wa korosho.
Amesema siku ya Korea wamekuja na utamaduni wa Tanzania na Jamhuri ya korea kuonesha tamaduni mbalimbali ikiwemo kuonesha mavazi ya kiutamaduni.
Kwa upande wake Mshauri wa Siasa na Uchumi kutoka Ubalozi wa Korea, Hyunseok Jeong amesema Leo ni siku muhimu kwasababu ni mara ya kwanza kushirikiana na Tantrade ikiwemo biashara na utamaduni.
“Inakumbukwa Juni mwaka huu Rais Dk.Samia Suluhu Hassan Suluhu alitembelea Jamjuri ya Korea hivyo uhusiano wa nchi hizi mbili ni mzuri wataendelea kushirikiana na wafanyabiashara wa Tanzania na kubadilishana uzoefu,”amesema.