Serikali inarajia kukamilisha ujenzi wa vyuo vya Veta 145 ifikapo mwaka 2025 kwa lengo la kuwawezesha kupanuzi wa mafunzo kwa kila mtanzania ili aweze kupata mafunzo mbalimbali kutokana na uhitaji wake.
Akizungumza katika maonyesho ya sabasaba katika banda la Veta,Mkadiriaji Majengo Sospeter Mgashe alisema kuwa awali vyuo vya Veta vilikuwa 51 baada ya bajeti viliongezeka vyuo 29 vya ngazi ya mkoa na wilaya ambapo vyuo 4 kwa ngazi ya mkoa na 25 kwa ngazi ya Wilaya,vyuo hivyo vinne kwa mkoa wa Njombe,Simiwihu na Geita mradi huo wa ujenzi ulikamilika mwaka 2022 .
Mgashe alisema kuwa vyuo hivyo vinaweza kudahiri wanafunzi kuanzia 500 hadi 600 kwa vitengo mbalimbali ndani ya vyuo vya Veta.
Mwaka 2023 serikali ilitenga bajeti ya ujenzi wa vyuo vipya 65, vyuo 64 vya wilaya na chuo kimoja cha mkoa wa Songwe kwa kuwa ulikuwa mkoa mpya kufikisha Veta kuwa na vyuo 145 nchi nzima
Alisema kuwa serikali inatambua kuwa vijana wanataka kuwa na ajira hivyo kuanzia vyuo vya Veta kutasaidia wananchi kujiajiri.
Mgashe alisema kuwa Veta itazalisha wataalam mbalimbali ambao hata mwekezaji akija Tanzania hawezi kukosa wataalamu kwenye uwekezaji wake.
Alisema kuwa wataalamu wanatoka katika vyuo vya Veta watasaidia kukuza maendeleo ya taifa kutokana na vijana watakaotaka kwenye vyuo hivyo kuweza kujiajiri wenyewe na kuajiri watu wengine.
Mgashe alisema kuwa hadi kufika mwaka 2022 Veta walikuwa na vyuo 80 kutoka vyuo vya awali 55 hivyo ilikuwa hatua kubwa sana kwa maendeleo ya vijana
” Tumeona serikali inavyopambana kuhakikisha vijana wanapata ajira kupitia Mafunzo wanayoyapata kupitia VETA hivyo Serikali inahakikisha kuna kuwa na wajuzi kila eneo la nchii hii”amesema Sopseter Mgashe mkadiriaji majengo.
Pia ameongeza kuwa Serikali imetoa fedha kwa ajili ya jengo la kusaidia kuratibu shughuli zote za VETA jijini Dodoma ambalo litakuwa makao makuu na ujenzi wake umefikia 28 na unatarajiwa kukamilika 2025 .
Aidha amesema kuwa Serikali inandaa utaratibu wa kufanya tafiti katika kuhakikisha wanatoa kipaumbele katika masomo ya tehama ili kujikita zaidi katika uboreshaji wa taaluma Kisasa.
Alimalizia kwa kusema kuwa vyuo vya Veta vipo katika ngazi ya mkoa wa wilaya zote nchi nzima ikiwa na lengo la kukuza ujuzi na kuleta maendeleo kwa Taifa na mtu mmoja mmoja kutokana na ujuzi walionao.