*Apongeza Wataalam Wizara ya Nishati/Taasisi kwa kutoa huduma bora kwa wananchi SABASABA
*Asema ni sehemu sahihi ya kupata mrejesho wa utendaji kazi*
*Ataka wadau wa Nishati Safi ya Kupikia kuwa na kanzidata*
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga amewataka Wataalam katika Wizara ya Nishati na Taasisi zake kujikita katika kufanya kazi kwa kasi, umakini na bidii ili kuwafikishia wananchi nishati ya uhakika na kwamba hicho ndicho kiwe kipimo kikuu cha kutangaza kazi za Wizara kwa wananchi.
Kamishna Luoga amesema hayo wakati alipotembea Banda la Wizara ya Nishati na Taasisi zake katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (SABASABA) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
“Sisi Wizara ya Nishati tumejipa changamoto ya kuongeza bidii zaidi ya kufanya kazi na kutoa huduma bora kwani Watanzania wanachotaka ni nishati ya kutosha ikiwemo ya umeme bila kuwa na usumbufu wowote.” Amesema Mha.Luoga
Ameeleza kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuhakikisha kuwa inatoa fedha za kutekeleza miradi ya uzalishaji, usafirishaji, usambazaji umeme pamoja na miradi mingine ya Nishati akitolea mfano mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) unaotekelezwa kwa kiasi cha shilingi trilioni 6.5 ambao sasa umefikia asilimia 98.
Ametaja baadhi ya miradi mingine ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa kuwa ni pamoja na ya usafirishaji umeme itakayounganisha Mkoa wa Katavi na Kigoma kwenye gridi ya Taifa ambayo ni mradi wa usafirishaji umeme kutoka Tabora hadi Katavi na Tabora hadi Kigoma pamoja na miradi ya kuboresha upatikanaji umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Kuhusu Maonesho ya SABASABA amesema “nimetembelea mabanda ya Maonesho ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake na kuona jinsi Wataalam wanavyohudumia wananchi kwa umahiri na kutoa huduma mbalimbali ikiwemo za kuunganisha umeme kupitia mfumo wa Nikonekt, kuonesha