Mwenyekiti wa umoja wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Mkoani Mara Mary Daniel amewataka vijana kushiriki Jogging pamoja na shughuli za maendeleo huku wakijua wanajukumu kubwa la kuhakikisha Usalama wa Taifa lao ikiwemo kutokujiingiza katika makundi mabaya.
Kauli hiyo ameitoa mara baada ya Jogging ilifanyika Mkoani mara ikiwahusisha viongozi wa Chama hicho ngazi ya Mkoa na wilaya ambapo amelitaka kundi hilo kutokutumika kinyume na malengo ya serikali.
“Vijana tujikiteni kushiriki shughuli za maendeleo tusitumike na Sisi tunawajibu nakuhakikisha tunashiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaaa kikamilifu ikienda sambamba nakuhamasiisha watu kujindikisha katika Daftari la mpiga Kura kuhakiki Taarifa zetu”Alisema Mary mwenyekiti wa UVCCM Mara.
Pia amewahikikishia vijana wasio wachama cha Mapinduzi hakuna kijana Mkoa wa mara atahayebaguliwa katika kuyafikia malengo yake.
Katika hatua nyingine katibu wa CCM Mkoa wa Mara Ibrahim mjanakheri amemtaka katibu umoja wa Vijana Mkoa huo kuhakikisha Zoezi la Jogging linaenda katika Wilaya zote za Mkoa wa Mara pamoja na kuhakikisha vijana wanashiriki katika usafi kwenye maeneo hayo.