Na Sophia Kingimali.
Katibu Mkuu Wizara ya kilimo Jerald Mweli amewataka vijana kuchangamkia fursa zilizopo katika miradi ya kilimo ili kujitengenezea ajira ya kudumu.
Mweli amesema hayo katika kongamano la vijana wanaojishughulisha na kilimo nchini lililoandaliwa na shirika la mageuzi ya kijana Tanzania(AGRA) kupitia mradi wa Building a Better Tomorrow (BBT)Julai 5,2024 uliohudhuriwa na vijana 100 toka mikoa mbalimbali Nchini.
“Wizara ya kilimo kwa kushirikiana na Asasi zisizo za kiserikali tumeandaa mpango maalumu kuhakikisha vijana wanajitengenezea ajira ya kudumu kupitia kilimo,na sasa hivi International Forum zote zitahusisha vijana ambapo vijana watakuwa wakisafiri nje ya nchi ili wakajifunze namna ya kuwekeza kwenye kilimo,nitoe wito kwa vijana jiajilini kwenye kilimo kilimo kina lipa na sasa hivi baadhi ya mashirika toka mataifa ya nje yanataka kuleta fund kwa ajili ya vijana wa kitanzania wanaojihusisha na kilimo”Amesema Mweli.
Mkurugenzi Mkazi wa shirika la uboreshaji wa kijana Tanzania (Agra) Vianey Rweyendela amesema kukua kwa uchimi wa Tanzania uliofikia 5.1% kwa mwaka kunatokana na shughuli za kilimo.
Akizungumza katika kongamano la vijana wanaofanya kazi za kilimo nchini Rweyendela amesema kukua kwa uchimi w Nchi umetokana na kilimo kwani 65%ya watanzania wanaishi kwa kutegemea kilimo.
Amesema katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan Bajeti ya kilomo imeongezeka zaisi ya mara 5 tofauti na vipindi vilivyopota na kwamba lengo la kuongeza bajeti ni kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kwamba Agra kupitia mradi wa BBT imelenga kusaidia vijana wakulima katika upatikanaji wa Masoko,madhamba na kuwakopesha fedha ili waweze kufanya shuguli za kilimo.
Nae mkurugenzi wa Kikombo Avocado Farm Emmanuel Kisinda Amesema tunawahamasisha Vijana kuingia Katika kilimo,kitu ambacho ni uti wa mgongo lakini Kupitia matamasha mbalimbali tunanufaika Kwa kupata vile vitu ambayo Vijana walikuwa wakidhani watavipata nyumbani lakini Kupitia mitandao ya kijamii tunakuwa tunawavutia watu wengi kama hivi wametualika Agra kuongelea Vijana ambao wapo Tanzania Kwa ajili ya mradi mkubwa ambao unakuja kutengeneza ajira Zaidi ya Milioni 1 kutoka Katika sekta ya kilimo
nikiwa kama kijana nimeajili Zaidi ya Vijana 50 Katika Shughuli zangu tofauti tofauti za shambani Kwa ajili ya kuajili ya Vijana wengi Zaidi Kwa kutanua biashara zetu wizara ya kilimo”. Amesema Kisinda