Na Mwandishi Wetu,Dar Es Salaam.
BOHARI ya Dawa Tanzania (MSD) kupitia Kampuni Tanzu yake ya MSD Medipharm Limited wamezindua kiwanda cha mipira ya mikono maarufu kama Gloves Makambako Mkoani Njombe ikiwa kuunga mkono juhudi za Serikali kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za Afya nchini.
Hayo yalisemwa leo Kaimu Meneja wa Bohari wa Dawa nchini (MSD) Medipharm Limited Omariy Magoolo aliyasema hayo katika maonyesho ya 48 ya baishara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa Road Jijini Dar es Salaam Julai 6,2024.
Ambapo akizungumza na waandishi wa habari alieleza kuhusu utekelezaji wa viwanda vya Bohari ya Dawa nchini (MSD) kimoja cha kikiwa Njombe na kinachojengwa Simiyu.
Alisema wameamua kufanya uwekezaji huo ili kwenda kuunga mkono jitihida za serikali za muda mrefu kuimarisha upatikanaji wa bidhaa hizo na mipango iliyopo yapo maeneo walioyachagua ikiwemo wilaya ya Kibaha Segereni Pwani ambako wanatarajia kuweka kiwanda kikubwa cha kuzalisha dawa na vifaa tiba.
Aidha alisema kwamba hivi sasa wapo kwenye hatua za mwisho kutekeleza mchakato huo na kila kitu kipo sawa huku akieleza eneo nyengine la uzalishaji wa bidhaa za tiba zinazotokana na malighafi za Pamba ikiwemo Bandeji, Ngozi ambacho watakifanya wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu kuna eneo hivyo mipango ya mbeleni.
“Rais Dkt Samia Suluhu amesisitiza ushirikiano wa serikali na Sekta Binafsi hivyo tupo kwenye maonyesho haya kwa sababu mbili kwenye kutoa elimu, ufananuzi kuhusu majukumu ya MSD na kuangalia washirika ambao tunaweza kushirikiana nao kwa namna moja au nyengine “Alisema
Aidha alisema hivi sasa barakoa zinazozalishwa na Bohari hiyo zinatumika kwenye migodi na viwanda hizi na sio hospitali wanaweza kuja wakauziwa na kuna makampuni ambayo yananunua na kusambaza maeneo mengine wanaweza kwenda kukutana nao ili kuweza kuona namna ya kuwauzia kwa bei ndogo ili kuweza kupata kwa gharama nafuu waweze kupelekea maeneo mengine.
Hata hivyo alisema kwamba kampuni hiyo tanzu inamilikiwa MSD kwa asilimia 100 na ilisajiliwa ramsi Aprili 2023 na bodi yake ilizinduliwa 20 June mwaka huu na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
Alieleza kwamba Bohari ya Dawa (MSD) ilikuwa na majukumu makuu matatu, kununua, kutunza na kusambaza dawa na vifaa tiba na mwaka 2021 kufuata mabadiliko ya kisheria ya MSD ambayo wakaongezewa jukumu la uzalishaji.
Alisema baada ya kupatiwa jukumu hilo Mejimenti ya MSD wakaona ni busara wakaipa kipaumbele mahuhusi kwa kuanzia kampuni tanzu iliyojikita kwenye viwanda kusimamia vilivyopo na kuibua viwanda vipya na kuendeleza.
Hata hivyo alisema kwamba awali walianza na kiwanda kimoja ambacho kinazalisha barakoa kipo Dar na baadae wakaongoza bidhaa nyengine ni barakoa maalumu kwa ajili ya magonjwa yanayoambukiza