Jaji Mafawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi Mhe. Jaji Dkt. Yose Joseph Mlyambina (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mawakili wa Serikali wakati alipotembelea banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali liliko kwenye maonesho ya Sabasaba yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi Mhe. Jaji Dkt. Yose Joseph Mlyambina akitia saini kwenye kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi Mhe. Jaji Dkt Yose Joseph Mlyambina (kushoto) akipokea vipeperushi kutoka kwa Wakili Serikali Mwandamizi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi Angella Kimaro (kulia)
……………….
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divishei ya Kazi Mhe. Jaji Dkt. Yose Joseph Mlyambina ameipongeza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kwa kutoa Miongozo mbalimbali ya Kisheria.
Mhe. Mlyambina ameyasema hayo alipotembelea banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema miongozo hiyo itawasaidia wadau mbalimbali wa sheria.
“Niwapongeze kwa kutoa miongozo hii, ni imani yangu sasa wadau wa sekta ya sheria wataifuata miongozo na itawasaidia katika kuboresha utandaji kazi wao”. Amesema Mhe. Mlyambina
Pia alipongeza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria kwa kutoa Jarida maridhawa lijulikanalo kama “Brain behind legislative Drafting in Tanzania”
“Niwapongeze pia kwa kuanzisha jarida hili natumaini wananchi hasa wadau wa sheria watajifunza mengi kuhusu nyinyi kupitia jarida hili,” alisema Mhe Mlyambina.
Awali akimkaribisha Mhe. Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Wakili Serikali Mwandamizi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Kimaro alieleza kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imetoa Miongozo na nyaraka mbalimbali.
Miongozo iliyotolewa ni kama vile Mwongozo wa utoaji wa ushauri wa Kisheri, Mwongozo wa Mikataba, Mwongozo wa Kamati za ushauri wa Kisheria za Wilaya na Mikoa, Mwongozo wa utengenezaji wa Sheria ndogo za Mamlaka za Serilali za Mitaa, Mwongozo wa Uandishi wa Sheria.
Pamoja na Miongozo hiyo Ofisi hiyo pia imetoa majina ya Sheria kwa lugha ya kiswahili, na istilahi za Kisheria, nyaraka hizi zinalenga kuboresha utendaji kazi katika Sekta ya Sheria