Mbunifu wa mashine ya kutengenezea chakula cha samaki Asusa Kumbukumbu kutoka Chuo cha ufundi VETA Songea amesema ubunifu wa mashine hiyo umekuwa mkombozi kwa vijana wengi kwani inaenda kuwa mkombozi wa ajira na kipato cha ziada kwa wafanyakazi.
Akizungumza katika banda la VETA lililopo kwenye maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa amesema mashine hiyo inatengeneza chakula cha mifungo kilichokuwa kwenye mfumo wa punje punje.
Amesema chakula hiko kinatumiwa na Kuku,Sungura na samaki ambapo baadhi ya samaki wanakula chakula kinachoelea ambao kati yao ni sato na wengine wanakula chakula kilichozama ambao samaki hao ni kambale.
“Tumebuni mashine hii kwa sababu watu wengi walikuwa wanapata tabu kutengeneza chakula cha samaki na kuku wakati malighafi ya kutengeneza chakula hicho inapatikani kwenye maeneo yao”,Amesema.
Ameongeza kuwa mifugo ambayo itapatiwa chakula hicho itakuwa na afya lakini pia itasaidia watu kuendelea kujiajili.
Sambamba na hayo kimaro ameishukuru taasisi ya sayansi na Teknolojia COSTECH kwa kuwa wadau wakubwa kwani ndio waliowafadhiri katika upatikanaji wa mashine hiyo ya chakula cha samaki.