…………………
Wanafunzi wanaosomea kilimo katika chuo cha Borigaram kilichopo kigamboni Dar es salaam, wametembelea banda la TFRA katika maonesho ya sabasaba kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali kuhusu tasnia ya mbolea
Katika banda la TFRA wanafunzi hao walipata fursa ya kuuliza maswali, wakijikita zaidi katika biashara ya mbolea na uwekezaji wa viwanda vya ndani vya mbolea.
Mmoja wa wanafunzi hao Gebinus Ndehele, ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kwa kutoa elimu ya mbolea kwa ujumla kupitia maonesho hayo.
Aidha Ndehele amesema kupitia elimu waliyopewa na wataalam wa TFRA kwenye maonesho ya sabasaba itakwenda kuwaongezea ufahamu katika masomo yao hususan kwenye mbolea
Maonesho hayo yanaendelea yakitoa fursa kwa wataalam wa TFRA kuitangaza taasisi na fursa mbalimbali zilizopo katika biashara ya mbolea na uwekezaji katika viwanda vya mbolea.