Mkuu wa mkoa wa Mara Kanal Evans Mtambi ameongoza zoezi la kusikiliza na kutatua kero za wananchi ofisini kwake ikiwa ni utaratibu aliouweka WA kusikiliza kero kila ijumaa.
Mkuu wa Mkoa wa Mara aliunda kamati ya kusikiliza na kupitia kero ambazo zimekuwa zikifika Ofsini kwake pamoja na kufika katika maeneo yanayolalamikiwa ili kujiridhisha kisha kutoa maaamuzi kwa kushirikisha pande zote mbili.
“Huu nimwendelezo wakusikiliza na kutatua kero za wananchi nakuzitolea maaamuzi papo hapo Kwa kushirikisha pande zote mbili ambazo zinahusiana”Alisema Kanal Evans Mtambi Mkuu wa mkoa wa Mara
Akizungumza mwenyekiti wa kamati hiyo iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanal Evans Mtambi, Pius Songoma Alisema tayari wameshasikiliza malalamiko ya 23 kwa kipindi cha wiki tatu.
“Tumefanikiwa kuwasikiliza hadi sasa wananchi 23 kwa kipindi cha wiki tatu na tumekuwa tukifanya hivi jumanne tunawasikiliza wananchi na ijumaa tunakutana na Mkuu wa mkoa kumpa mrejesho”Alisema Pius Songoma mwenyekiti wa kamati ya kusikikiza kero ofisni kwake.
Aidha baadhi ya wananchi wamempongeza Mkuu wa mkoa mara kwa kuja na mpango huo kwani utasaidia kutatua migogoro inayofika katika ofisi ya mkuu wa mkoa.