Waziri wa nchi ofisi ya Rais ,Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza Mkoani Arusha alipotembelea hoteli ya Parrot.
Mwenyekiti wa bodi ya Hoteli ya kitalii ya Parrot ya Jijini Arusha, Abdallah Msele akizungumza Mkoani Arusha.
……….
Happy Lazaro, Arusha .
Waziri wa nchi ofisi ya Rais ,Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo, amepongeza uwekezaji wa Mradi mkubwa wa hoteli ya Parrot uliofanywa na wazawa na kuwa ni kielekezo kizuri na mfano wa kuigwa na wengine .
Ameyasema hayo leo kwenye hafla fupi ya kutembelea mradi huo wa hoteli iliyopo barabara kuu ya col .milditon kata ya kaloleni, na kusema kuwa uwekezaji wa Mradi huo ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika swala Zima la Utalii.
Amesema changamoto zilizopo zitaendelea kufanyiwa kazi ili kuendelea kutoa unafuu kwa wawekezaji wa miradi mbalimbali nchini na kuendelea kuwekeza zaidi kwa maslahi ya nchi na kutoa ajira nyingi kwa wazawa.
“Kwa kweli nimefurahishwa sana na huu uwekezaji uliofanywa na hawa wazawa kwani wameonyesha nia ya kuendelea kumuunga mkono Rais Samia hasa katika sekta ya utalii kwani uwepo wa hoteli hii unatoa fursa ya kuendelea kuvutia watalii kuja kwetu.”amesema Prof.Mkumbo.
Kwa upande wake meneja wa benki ya Uwekezaji TIB,Samweli Michael Minja,amesema wametoa ufadhili wa Mradi huo ili kusaidia kukamilisha Mradi huo unaotekelezwa na wazawa.
Naye Mwenyekiti wa bodi ya Hoteli ya kitalii ya Parrot ya Jijini Arusha, Abdallah Msele,amesema mradi huo wa hoteli umekamilika kwa 98% na unatoa ajira rasmi 200 na zisizo rasmi 300 .
Amesema Mradi huo ulianza mwaka 2004 ulikumbwa na changamoto na ulisimama hivyo mmiliki wake wa awali marehemu,Abdallah Idd Mshana,aliomba mikopo benki ya Uwekezaji na mitaji TIB,iliyotoa mikopo uliowezesha ujenzi kuendelea.
Msele,amesema kuwa hoteli hiyo itakuwa na Vyumba 116,migahawa mitatu na kumbi 9 za mikutano,hivyo kuwataka wadau mbalimbali kuwaunga mkono ili kuendelea kumuunga mkono Rais Samia.
Ameomba mifumo kati ya mamlaka ya mapato nchini TRA na Kituo cha uwekezaji TIC uwe inasomana Ili kuwaondolea usumbufu Wawekezaji wa miradi mikubwa