Na Sophia Kingimali.
Mkurugenzi Mkuu Tume ya Ushindani Nchini (FCC ) William Erio amesema kufuatia na kuwa na mazingira mazuri yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya usimamizi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan umepelekea nchi kuwa sehemu sahihi ya uwekezaji.
Hayo ameyasema leo julai 3,2024 wakati alipotembelea banda la tume hiyo katika maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa ambapo mwaka huu yanabebwa na kauli mbiu isemayo ‘Tanzania ni mahali sahihi kwa biashara na uwekezaji’.
Amesema sera nzuri za uwekezaji zilizopo nchini ni kichocheo kikubwa cha uwekezaji lakini pia upatikanaji wa malighafi na uwepo wa miundombinu kam maji,umeme na usafirishaji vimeweza kuchochea uwekezaji.
“Katika sensa iliyofanyika mwaka 2020 nchini tupo watanzania zaidi ya milioni 60 hivyo muwekezaji anapokuja nchini anauwakika wa kupata nguvu kazi”,amesema.
Amesema pamoja na mambo mengine jambo linalovutia zaidi uwekezaji na kurahisisha ufanyaji wa biashara ni kuwa na taasisi za usimamizi wa shughuli za kibiashara ambazo zipo imara.
Ameongeza kuwa iwapo taasisi zitahakikisha na kusimamia vizuri hakuna mfanyabiashara atakaefanya biashara kwa kutumia mbinu chafu na adaifu wala kufanyabiashara kwa kutumia bidhaa bandia.
“Yote haya yatawezekana kama FCC watafanyakazi yao vizuri pamoja na kuchukua hatua za kusimamia kwani hayo ni moja ya majukumu yao na ndio maana tupo hapa pia kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma”,Amesema.
Aidha Erio ametoa rai kwa wananchi wote wakiwemo wafanyabiashara kufika katika banda lao ili wapate elimu ili waepuke kujishighulisha na bidhaa bandia na vitu vingine ambavyo haviruhusiwa na sheria ya ushindani.
“Tunataka wafanyabiashara wafanye biashara za halali ili wananchi wanufaike na biashara hizo lakini serikali ipate mapato na tupo tayari kutoa elimu katika kipindi chote cha maonesho”,Amesema.