Viongozi wa shirikisho la vyama vya wafanya kazi Mkoani Mara wamejitokeza hadharan kumshuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kuongeza asilimia ya utoaji wa mafao ya mkupuo (kikokotoo) kutoka 33% kwenda asilimia 40.
Akizungumza kwaniaba ya wafanya kazi mratibu wa Tucta Mkoa wa mara mussa mashamba amesema kitendo kilichofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan sikwamatakwa yake bali nikisikio na kutatua kilio kikubwa cha watumishi waliokuwa nacho.
“Huyu nimama amesifia kilio cha Muda mrefu chakwamba wastaafu walikuwa Wanastaaf lakini mafao yao ya mkupuo yalikuwa kidogo ametusikia na sasa amekubali kuongea kwakweli nijambo la kupongezwa sana kwa mama huyu”Alisema Mussa mashamba mratibu wa Tucta Mkoa wa mara.
Pia Musa Alisema kuwa maneno mengi yamekuwa yakizungumzwa juu ya Jambo hilo lakini wenye namna yakulizungumza niwatumishi na siwatu wengine ambapo kwa sasa wanachakujivunia kama watumishi.