NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO
Tafiti zinaonesha kundi kubwa la Vijana wenye umri wa miaka 15-24 wapo hatarini kupata maambuki mapya ya virusi vya UKIMWI kutokana na kundi hilo kutokuwa tayari kupima na kujua afya zao.
Cyprian Komba Meneja wa Utetezi na Habari Mtandao wa vijana wanaoishi na virusi vya UKIMWI Tanzania anasema utafiti uliofanywa na serikali kwa mwaka 2022-2023 unaonyesha maambuki mapya ya virusi vya UKIMWI ni watu 60000 na asilimia 40% kundi la vijana wenye umri wa miaka 15-24 na karibia aslimia 80% kati hiyo arobaini ni mabinti wakike wanaongoza kuwa na maambukizi mapya.
Komba ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye kongamano la kujadili hali ya maambukizi ya virusi vya UKMWI kwa wanafunzi wa vyuo vikuu lililofanyika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Kampasi Kuu ya Edward Moringe Mkoani Morogoro.
“Tunaona kuwa idadi hiyo ni kubwa kwa pamoja wadau na serikali tunashirikiana kutoa elimu kwa vijana waliopo kwenye Vyuo Vikuu na kuhakikisha kundi hilo linakuwa tayali kupima virusi vya IKIMWI na kujua afya zao,” amesema
Kwa upande wake Afisa Tathimini na ufuatiliaji kutoka NACOPA Japhet Kakwezi amesema programu ya kutoa elimu kwa kundi la vijana wenye umri wa miaka 15-24 ambao wapo hatarini kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI ni endelevu lengo vijana waweze kupima na kujua afya zao.
“Kuna changamoto kubwa iliyopo kwa kundi hili la vijana ni vijana wengi hawapo tayari kupima na kujua afya zao kwa hiyo wito kwa wadau pamoja na serikali kushirikiana na kwa pamoja kutuweze kutoa elimu kwa kundi hili la vijana”.
Aidha Kakwezi amesema mpaka sasa taasisi hiyo imetoa elimu kwenye vyuo vikuu 10 na halmashauri mbalimbali Tanzania nzima na kushirikiana na watu wanaoishi na virusi vya hivyo katika upimaji .
Chery Holister ni mhamasishaji jukwaa la vijana wanaoishi na virusi vya UKIMWI Tanzania, NACOPHA amesema, vijana wengi wanakwepa kupima virusi vya UKIMWI na kujua afya zao kutokana na unyanyapaa kwa jamii hivyo kuiomba jamii kuona ugonjwa huo kama ugonjwa mwingine na kuacha kutenga wagonjwa na kushirikiana nao katika mambo mbalimbali.
Norah Macha ni mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo SUA amesema elimu waliyoipata itawasaidia kujua afya zao na kufikia malengo waliyojiwekea huku akiushukuru Iongozi wa SUA, pia ameishukuru taasisi hiyo kwa kuandaa kongamano hilo