Kaimu Meneja wa kiwanda cha kuzalisha mpira ya mikono cha MSD kilichopo Idofi, Makambako mkoani Njombe Bw. Shiwa Mushi akitoa maelezo kwa wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea kiwanda hicho mkoani Njombe ili kujifunza na kuona shughuli zake.
Afisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka akiwafafanulia wahariri wa vyombo vya habari mambo mbalimbali mara baada ya kutembelea kiwanda hicho.
………………
MATUNDA ya kuanzishwa kwa Kampuni Tanzu ya MSD Medipham Manufacturing CO LTD, yameanza kuzaa MATUNDA baada ya kiwanda cha kuzalisha mpira ya mikono cha MSD kilichopo Idofi,wilayani Makambako mkoani Njombe kuwa mbioni kuanza rasmi kuuza bidhaa hizo kwa wadau mbalimbali hivi karibuni.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kiwanda hicho kuanza uzalishaji Februali , mwaka huu ambapo tayari kimezalisha jozi (pear) milioni 2 Hadi sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho kinachomilikiwa na Bohari ya Dawa (MSD) kupitia kampuni yake tanzu hiyo, Kaimu Meneja wa kiwanda hicho, Shiwa Mushi, alisema kina uwezo wa kuzalisha jozi 10,000 kwa saa
Mbali na kampuni tanzu hiyo kumiliki kiwanda hicho, inamiliki viwanda vingine viwili ambavyo vipo hatua za mwisho kuanza uzalishaji.
Viwanda hivyo ni kiwanda cha kuzalisha bidhaa za pamba kilichopo Simiyu na Zengereni cha Pwani ambacho kitakuwa kinazalisha dawa
Kwa mujibu wa Mushi, kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha mipira ya mikono milioni 86.4 kwa mwaka sawa na asilimia 83. 4 ya mahitaji ya nchi.
Naye Afisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiruka, , alisema tayari wanaelekea kuanza kuuza bidhaa zake
Alisema kabla ya kuanzishwa kwa kiwanda hicho, MSD ilikuwa mdau mkubwa wa kununua bidhaa hizo, kuuza na kuzisamba kwa wadau, ikiwemo hosptali, vituo na zanahati.
Chimbuko la kuanzishwa kwa Kiwanda hicho ni mwaka. 2020, ambapo Dunia ilikumbwa na ugonjwa wa COVID 19, hivyo kuathiri upatikanaji na usambazaji wa Dawa na vifaa Tiba duniani na hapa nchini
Hali hiyo iliisukuma Serikali kupitia MSD Kuwa na Mkakati wa kuzalisha vifaa Tiba na Dawa, ili kujiweka tayari iwapo Changamoto Kama hiyo itajitokeza ikute nchi imejiandaa kuhudumia wananchi wake kwa kupata Dawa na vifaa tiba