Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Ali Mohammed Shein amepokea taarifa ya maendeleo ya Chuo hicho kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Prof. WilliamNMwegoha iliyoangazia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Chuo kwa mwaka 2023/2024. Dkt. Shein amepokea taarifa hiyo Ofisini kwake katika eneo la Mazizini Zanzibar.
.Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Saida Yahya – Othman akitoa neno la utangulizi wakati wa kukabidhi taarifa ya maendeleo ya Chuo kwa
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha akikabidhi taarifa ya maendeleo ya Chuo kwa Mkuu wa Chuo na Rais Mstaafu wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha akisoma taarifa ya maendeleo ya chuo kwa Mkuu wa Chuo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la
Chuo, Prof. Saida Yahya – Othman na kulia Naibu Makamu Mkuu Wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Allen Mushi.
Picha ya pamoja ya Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali
Mohamed Shein (Katikati) na viongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe mara baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya Chuo Kikuu Mzumbe. Dkt. Shein amepokea
taarifa hiyo Ofisini kwake katika eneo la Mazizini Zanzibar
……….
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amepokea taarifa ya maendeleo ya Chuo iliyowasilishwa na Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha tarehe 01 Julai 2024 Zanzibar.
Katika kuwasilisha taarifa hiyo ya maendeleo kwa kipindi cha miezi sita (Disemba 2023 hadi Juni 2024), uongozi wa Chuo umeongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Prof. Saida Yahya – Othman, Makamu Mkuu wa Chuo Prof. William Mwegoha na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Mipango, Fedha na Utawala) Prof. Allen Mushi.
Taarifa hiyo iliyowasilishwa mapema leo imejikita kueleza hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Chuo Kikuu Mzumbe, ikiwa ni pamoja na taarifa za utekelezaji wa miradi ya Chuo kwa fedha za ndani, hali na ustawi wa Watumishi na Wanafunzi, kujenga uwezo wa watumishi wa Chuo, kuimarisha ushirikiano na wadau wa ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kusaini hati za makubaliano ya ushirikiano na mashirika, Taasisi na Vyuo Vikuu vya nje ya nchi.
Aidha kupitia taarifa hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo ameeleza juu ya miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa na Chuo kwa ufadhili wa Serikali, akiutaja mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) na kueleza namna ambayo Chuo Kinaendelea kunufaika kupitia mradi huo pamoja na matarajio yake huku akieleza nia ya dhati ya uongozi wa Chuo katika kuendelea kusimamia kwa weledi hatua za utekelezaji wa mradi huo.
Vilevile, Makamu Mkuu wa Chuo ameeleza hatua za maandalizi ya Mahafali ya 23 na kwamba baraza la chuo na menejimenti wanaendelea kufuatilia hatua za maandalizi ili kuleta ufanisi wa mahafali hayo.
Akizungumza na viongozi hao Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Ali Mohamed Shein ameeleza namna alivyofurahishwa na jitihada zinazofanywa na Chuo hasa katika utekelezaji wa miradi, kuanzisha ushirikiano na taasisi nyingine pamoja kutambua na kuthamini hali za wafanyakazi kwa kuwapandisha vyeo wale wote wanaostahili.
Aidha amewataka viongozi wa Chuo kuendelea kufanya kazi kwa bidiii na maarifa ili kufikia malengo yaliyoaainishwa katika Mpango Mkakati wa chuo.
Vilevile, Makamu Mkuu wa Chuo ameeleza hatua za maandalizi ya Mahafali ya 23 na kwamba baraza la chuo na menejimenti wanaendelea kufuatilia hatua za maandalizi ili kuleta ufanisi wa mahafali hayo.
Akizungumza na viongozi hao Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Ali Mohamed Shein ameeleza namna alivyofurahishwa na jitihada zinazofanywa na Chuo hasa katika utekelezaji wa miradi, kuanzisha ushirikiano na taasisi nyingine pamoja kutambua na kuthamini hali za wafanyakazi kwa kuwapandisha vyeo wale wote wanaostahili.
Aidha amewataka viongozi wa Chuo kuendelea kufanya kazi zaidi ili kufikia malengo yaliyoaainishwa katika mpango mkakati wa chuo.