NA BALTAZARMASHAKA, MWANZA
SHIRIKA la Kimataifala ICAP Tanzania,limempongeza Rais Dk.Samia Suluuhu Hassan kwa kuwekeza katikaelimu ya kudhibiti matumizi na uingizaji wa dawa za kulevya nchini.
Pongezi hizo limetolewaleo jijini Mwanza na Mkurugenzi Mkaazi wa ICAP nchini, Haruka Maruyama alipozungumzakatika kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya kupiga vita dawa za kulevya.
Amesema anampongezaRais Dk.Samia na Serikali ya Awamu ya Sita anayoiongozwa kwa kuwekeza katika elimu,Watanzaniawatakuwa salama kupitia elimu hiyo, watafahamua athari na madhara ya dawa zakulevya kiafya,kijamii na kiuchumi kwa sababu dawa hizo zina athari kwamtumiaji.
Maruyama amesemamaadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya ni mahususi katika kutafuta changamoto na mbinu za kupambana na dawa hizo kati ya serikalina wadau.
Mkurugenzi huyo waICAP nchini alisema ushirikiano kati ya serikali na mashirika mbalimbali yaliyokatika nyororo wa kupiga vita dawa za kulevya umeimarika sana.
Aidha ushirikianohuo umetoa fursa kwa mashirika hayo kutoahuduma za afya na elimu kwa waraibu wa dawa za kulevya ikiwemo kuwapa elimu yaujasirimali ili wakishapona wapate kazi ya kijiingiza kipato na kukukuza uchumiwao na taifa ka ujumla.
“ICAP kwa miaka 20tunatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii nchini Tanzania kupitia ufadhiliwa CDC na PEFAR,hivi karibuni serikali imezindua taarifa ya mradi wa utafiti waviashiria vya ukimwi na matokeo ya ukimwi (THIS 2020-2024) mkoani Morogoro,”amesemaMaruyama.
Amesema kupitia kiliniki ya Waraibu (MAT),jumla yawaraibu 770 wamehudumiwa kupitia methdone na waliokuwa wakisumbuliwa na matatizo ya afya ya akili wengi wakiwa niwaraibu wa dawa za kulevya wamenufaika kwa kupatiwa huduma ya matibabu ambapokwa sasa tatizo hilo limepungua.
Maruyama ameahidikuwa ICAP itaendelea kushirikiana na serikali kufanya na kutafutawafadhili ili kuunga mkono serikali ya awamu ya sita kuleta maendeleo.