Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Kibakwe, Mhe.George Simbachawene akiweka shada la maua kwenye kaburi aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum wa Jimbo la Kibakwe, Mhe.Maria Kigosi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Mhe. George Fuime akizungumza wakati wa Ibada ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum wa Jimbo la Kibakwe, Mhe.Maria Kigosi iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kibakwe, Tarafa ya Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Kibakwe, Mhe.George Simbachawene akimfariji mmoja wa Mtoto aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum wa Jimbo la Kibakwe, Mhe.Maria Kigosi
Watoto wa aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum wa Jimbo la Kibakwe, Mhe.Maria Kigosi wakiweka shada la maua kwenye kaburi ya Mama yao mara baada ya mazishi yaliyofanyika Tarafa ya Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma
Baadhi ya ndugu wa karibu wa aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum wa Jimbo la Kibakwe, Mhe.Maria Kigosi wakiweka shada la maua kwenye kaburi ya Mama yao mara baada ya mazishi yaliyofanyika Tarafa ya Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya a yMpwapwa Mkoani Dodom
………
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Kibakwe, Mhe.George Simbachawene amesema aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum wa Jimbo la Kibakwe, Mhe.Maria Kigosi amekufa kifo cha kawaida na hakuna mtu yeyote aliyempa sumu.
Pia, amesema Marehemu hajafa kifo cha ghafla kama inavyodaiwa bali alikuwa anaumwa na amefia hospitali ya Tumaini Wilayani Mpwapwa.
Ametoa kauli hiyo leo wakati akishiriki Ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kibakwe, Tarafa ya Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Amefafanua kuwa Marehemu alikuwa anaumwa kwa muda mrefu ambapo watu wa karibu akiwemo Mume wa Marehemu anatambua kuwa Mke wake alikuwa akiumwa kwa muda mrefu na amekiri kuwa alikuwa mbioni kumpeleka Mke wake katika hospitali kubwa.
‘‘ Lakini huku mtaani kumekuwa na maneno mengi kuwa Marehemu alipewa sumu na wameenda mbali zaidi kwa kuwataja wahusika waliompa sumu na sumu hiyo ilitoka kwa nani, nataka niwahakikishie sio kweli ni huo uongo mtupu ” ameng’aka Mhe. Simbachawene.
Amesema kuna wengine wameanza kuthubutu hata kuwataja wahusika waliompa sumu hiyo huku akisisitiza wenye tabia hiyo waache mara moja kwani huo na hautawasaidia chochote
Aidha, ameweka bayana kuwa Serikali imefanya utafiti wake kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na familia yake hususani mume wake na kujiridhisha kuwa Marehemu Maria hakulishwa sumu.
Hata hivyo Mhe.Simbachawene amesema madaktari wameweza kujua alichokuwa akiumwa ndani ya muda mfupi aliokimbizwa hospitalini.
Kufuatia hatua hiyo, Mhe.Simbachawene amewataka Madiwani, Wananchi wa Kibakwe pamoja na familia yake kwa ujumla kupuuza uvumi huo la sivyo wataanza kugombana pamoja na kudhalilishana kwenye jambo lisilo na chembe chembe yoyote ya ukweli.
” Tutagawanyika, tutavunja umoja wetu tulioujenga kwa muda mrefu na tutaruhusu maadui kuingia bila sababu nataka niwahakikishie Maria ameondoka kwa kifo cha kawaida.
Mhe. Simbachawene amemuelezea Diwani Maria kama Kiongozi aliyependa kuunganisha watu na kuwaasa viongozi wengine kuna kitu cha kujifunza kutoka kwake.
Pia ametumia fursa hiyo kutoa pole kwa familia, Uongozi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mpwapwa, pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kuondokewa na Kiongozi mahiri.
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mhe, Maria Kigosi alifikwa na umauti siku ya jumatano saa kumi usiku mara baada ya kuanza kujisikia vibaya na kukimbizwa hospitalini ya Tumaini Wilayani Mpwapwa alikoenda kwa ajili ya kushiriki vikao vya Madiwani.