Kushoto meneja wa NHIF ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Dr. Raphael Mallaba akiwa na Meneja wa NHIF ofisi ya Ilala Dr. Aifena Mramba wakitoa elimu kwa wakaazi wa mtaa wa zakhem wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya NHIF KITAANI MWAKO iliyozinduliwa jana katika viwanja vya Zakhem jijini Dar es salaam jana.
Afisa wa bima ya afya mkoa wa Temeke Bi Mwamy Msamy akitoa elimu kwa mwananchi.
Bi Grace Kissinga Kaimu Meneja Uhusiano akiendelea kutoa elimu ya bima ya afya kwenye kata ya Mbagala jijini Dar es Salaam.
Wananchi tambueni kuwa kukata bima ya afya si tu pale unapougua au ndugu anapougua ndiyo tufikirie kwenda mfuko wa taifa wa Bima ya Afya NHIF ili uweze kukata Bima kwa ajili ya kupata huduma za afya unatakiwa kukata Bima kabla ya kuugua
Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya mkoa wa Temeke Bw. Canon Luvinga wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya uhamasishaji Wananchi kujua faida na umuhimu wa kujiunga na bima ya afya katka viwanja wa Mbagala Zakhem jijini Dar es salaam.
Amesema huu ni mkakati endelevu wa kuwafikia wananchi kwenye Kila kata na wilaya nchini kwani wananchi kuelimika kuhusu Bima ya afya ni jambo la kwanza na kufanya maamuzi ya kujiunga ni hatua nyingine kwani tumebaini wananchi wengi Wana uelewa mdogo kuhusu bima ya afya.
“Unakuta ndugu anakuja ofisini kuuliza gharama za kulipia bima ya afya wakati huo huo anakwambia huyu ni mgonjwa na tumejipiga hata hivyo tunaenda kuuza kiwanja Ili tumkatie bima ya afya,” Amesema Bw. Canon
Hili nalo limetusukuma kutoka ndani ofisini na kuja kumuelimisha mwananchi ili asiingie kwenye umasikini kwa sababu ya maradhi wakati bima ya afya ipo.
Ameongeza kuwa ni mafanikio makubwa kwa NHIF kupata idadi kubwa ya Wananchi waliojitokeza kushiriki uzinduzi wa kampeni hii kwani takribani watu 800 wamehudhuria, mbali ya elimu pia huduma za upimaji afya Bure kwenye magonjwa yasiyoambukiza zilitolewa na madaktari kutoka NHIF.
Watu 380 waliweza kupima afya zao kati yao 30 walibainika kuwa na dalili za magonjwa ya kisukari na presha hivyo walishauriwa kuhudhuria kwenye vituo vilivyo karibu kwa ufuataliliaji.
Hata hivyo watu 70 wamesajiliwa papo papo ambapo
NHIF ofisi ya Temeke imedhamiria kuhakikisha mwananchi anafahamu vyema faida na umuhimu wa kujiunga na bima ya afya kwani tumeona Kuna ombwe kubwa la uelewa kuhusu bima ya afya.
“Hivyo Mimi na timu yangu tumejipanga kutokukaa ofisini bali kwenda mtaani mwananchi aone ipo haja ya kujiunga na ukizingatia serikali inakuja na mpango wa bima ya afya kwa wote hii itasaidia kujenga uelewa zaidi.
Nao Wananchi walioshiriki katika uzinduzi huo wamekiri kuwa huu ni mpango mzuri kwani waliowengi wanaona bima ya afya ni gharama kubwa lakini kwa elimu tuliyoipata kwanza tunaweza kubana vipato vyetu kwa kudunduliza na kuweza kulipia bima ya afya kwani tumeambiwa unalipa mara moja unapata huduma mwaka mzima.