Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bwawani Kijitonyama ndugu Twaha John Leo alipata nafasi ya kugawa Reflector za Bodaboda wa Kata hiyo.
akizungumza katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikua Katibu Mwenezi Wa Mkoa wa DSM ndugu Ally Bananga ‘Binamu’ mtu Makini.
Amewaomba vijana madereva wa Bodaboda kuwa makini na kufanya kazi kwa bidii kwakuwa wao ni sehem mojawapo ya nguvu kazi ya taifa inayochangia kukuza uchumi katika eneo hili la Kijitonyama na Dar es salaam kwa ujumla katika suala Zima la usafirishaji,
Twaha John ameongeza kuwa ipo haja ya bodaboda wote kujisajili ktk makundi na kurasimisha maeneo yenu mnayofanyia kazi zenu Kila siku.
Hii ni wamu ya Sita ya Rais Mh. Dkt.Samia Suluhu Hassan nayo inawajali vijana na imetoa miongozo mizuri tu kwa Halmashauri zetu zote kutoa Mikopo kwa Vijana na vijana wenyewe ndo nyie.
Sisi viongozi na nyie Bodaboda tushirikiane kwa pamoja katika kuwa mfano wa kuigwa twendeni Kisasa Zaidi katika shughuli zetu Leo nimeanza na kugawa “Reflector” taratibu tutafanya na vingine vikubwa zaidi.
Nae Mgeni Rasmi Katibu Mwenezi Wa Mkoa DSM Ndugu Ally Bananga ‘Binamu’ amempongeza Mwenyekiti huyo Twaha John kwa jinsi anavyojishusha na kujiweka karibu na Vijana wenzie japo yeye ni Kiongozi, huo ndio Uongozi “Mwenyekiti Twaha John endelea hivyo na kama mtaona mtahitaji msaada wowote mimi nipo kama Mwenezi wa Mkoa ntafarijika Sana nikiona Vijana hawa wa Bodaboda wa hapa Kijitonyama Bwawani ndo mfano wa Bodaboda wote Mkoa wa Dar Essalam katika kutii Sheria za barabarani na kutii sheria bila shuruti.” Amesema Bananga.
Ndugu Ally Bananga ameishukuru Kampuni ya Refuelling Solutions ambao wao ndo wametoa msaada huo uliowasilishwa na Meneja Mkuu Ndg Renatus Mabeyo.
Awali akimkaribisha Mwenezi huyo Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kijitonyama Ndugu Ismail Mwenda ‘Suma’ aliwapongeza Bodaboda hao kwa kua mstari wa Mbele katika kutoa taarifa sahihi pindi wanapoona Kuna sintofahamu yoyote ile katika eneo hilo la Kijitonyama.
Msemaji wa Bodaboda hao ndugu Jaffari Kondo alimshukuru Mwenyekiti Twaha John kwa kuendelea kuwa karibu nao kwa Muda wote kwani “Reflector” hizo ni muhimu Sana kwao hasa usiku ili kuwaepusha na ajali.