Dawa (MSD),kusaidia serikali kudhibiti upatikanaji na uchepushaji wa dawa tiba zenye asili ya kulevya na kemikali bashirifu.Ametoa maagizo hayo leo katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza,alipotembelea na kukagua banda la MSD katika maadhimisho ya Siku ya Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya ambapo MSD ina jukumu la kuzalisha,kuhifadhi,kuuza na kusambaza bidhaa za afya zikiwemo
dawa tiba za asili ya kulevya.
Mhagama akiwa katika banda la Shirika lisilo la Kiserikali la ICAP nchini,alipata maelezo kutoka kwa vijana (mabalozi) waliokuwa waraibu wa dawa za kulevya ambao baada ya kutibiwa na
kupona kwa msaada shirika hilo wameajiriwa kuwa mabalozi wa kutoa elimu ya kupiga vita dawa za kulevya katika jamii.
Vijana hao wamemwomba Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,kupitia serikali anayoiongoza kuwapunguzia gharama za masomo hitajika vijana wanaoachana na matumizi ya dawa za kulevya ili waweze kujiunga na masomo ya fani zitakazowawezesha kujiajiri.
Waziri huyo wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na Uratibu ameahidi kulichukua ombi hilo na kulifanyia kazi ingawa awali vijana hao walipewa fursa kusoma katika vyuo vya ufundi stadi (VETA).
Mhagama alikuwa akikagua mabanda ya washiriki wa madhimisho ya Siku ya Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya yanayofanyika katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza,kilele ni