Happy Lazaro,Arusha .
Arusha.Wadau wa Afya kutoka mkoa wa Arusha na Manyara wamekutana mkoani Arusha kwa lengo la kujadili magonjwa yasiyoambukizwa na matibabu shufaa kutokana na magonjwa hayo kuwa changamoto kubwa katika jamii.
Aidha wadau hao wamekutana katika kongamano la kisayansi la Selian Lutheran Hospital katika kuadhimisha miaka 70 ya utoaji wa huduma katika hospitali hiyo.
Akizungumza katika kongamano hilo mkoani Arusha ,Mkurugenzi Mkuu wa Selian Lutheran Hospital ,Dk. Amon Marti amesema kuwa,tatizo hilo la magonjwa yasiyoambukizwa bado ni changamoto kubwa katika jamii kwani asilimia 80 ya wagonjwa wanaolazwa hospitali wanatoka na magonjwa hayo ndo maana wameweza kukutana na kuweza kuona upana wa ugonjwa na kuweza kuweka mikakati mbalimbali ya kudhibiti katika maeneo yao.
Dk.Marti amesema kuwa,lengo la kongamano hilo kuweza kujifunza kwa pamoja kuhusu magonjwa hayo na namna ya kuweza kuratibu .
“Katika kuadhimisha miaka 70 ya utoaji wa huduma katika hospitali yetu tumekutana ili kuweza kujitafakari na kuona tunafanyaje kama hospitali kwa kuwajengea uwezo watumishi wetu katika maswala mbalimbali ikiwemo kufanya tafiti mbalimbali. “amesema .
Aidha amewataka wananchi kufanya mazoezi kwa wingi ili kuweza kuondokana na magonjwa hayo pamoja na kuzingatia matibabu yanayotolewa na wahudumu wa afya katika vituo na hospitali mbalimbali.
“Bado tatizo ni kubwa katika jamii na hii inasababishwa na mfumo wa maisha ambao unabadilika kila siku katika jamii na kupelekea kuwepo kwa ulaji holela unaosababisha kuleta magonjwa hayo .”amesema.
Ameongeza kuwa ,kama hospitali wanajivunia kutoa huduma bora na kwa kiwango cha juu sana kwani walianza kama Zanahati na kuendelea kukua siku hadi siku kutokana na huduma bora,na hatimaye wakaendelea kukua hadi ngazi ya mkoa katika tiba shufaa na kuweza kutoa huduma za kibingwa.
Dkt.Marti amesema kuwa , wamejiwekea mikakati ya kuhakikisha wanaendelea kuimarisha huduma bora kwa wananchi pamoja na kuendelea kuwa na madokta bingwa wabobezi.
Naye Meneja masoko kutoka kampuni ya Action Medeor International Healthcare Tanzania ,Mary Tarimo ambaye ni miongoni kwa washiriki , amesema kuwa,kupitia kongamano hilo litaleta manufaa makubwa kwao katika kwenda kutoa elimu zaidi kwa jamii kuhusu kijikinga na magonjwa yasiyoambukiza sambamba na kutoa elimu jinsi ya kutumia vyakula na kujikinga na magonjwa hayo
“Kwa kweli tunashukuru sana Selian Lutheran Hospital kwa kutukutanisha katika kongamano hili kwani tumeweza kujifunza kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza na namna ya kuchukua tahadhari ili kuepukana na magonjwa hayo na tunaahidi kuwa mabalozi wazuri wa kutoa elimu hiyo kwa jamii yetu.”amesema.