Meneja ununuzi Mbolea kwa pamoja na Mchumi Mwandamizi Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) Elizabeth Bole akizungumzia ushiriki wao katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama sabasaba mwaka huu 2024 yanayofanyika jijini Dar es salaam.
Afisa biashara na Kaimu Meneja uzalishaji wa ndani na Mazingira Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) Getrude Ng’weshemi wakati akizungumzia ushiriki wao katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama sabasaba mwaka huu 2024 yanayofanyika jijini Dar es salaam.
Meneja Maabara kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) Leila Robin akizungumzia ushiriki wao katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama sabasaba mwaka huu 2024 yanayofanyika jijini Dar es salaam.
Meneja Uhusiano na Elimu kwa umma Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) Matilda Kasanga akielezea ushiriki wao katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama sabasaba mwaka huu 2024 yanayofanyika jijini Dar es salaam.
……………………..
NA MUSSA KHALID
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini- TFRA imeendelea kuwasisitiza wadau mbalimbali kutumia fursa mbalimbali za kuwekeza katika tasnia ya Mbolea nchini Ili kuongeza wigo wa Tanzania kuwa na uzalishaji mkubwa wa Mbolea ndani na nje ya nchi.
Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Meneja ununuzi Mbolea Kwa pamoja na Mchumi Mwandamizi TFRA Elizabeth Bole wakati akizungumza ushiriki wao katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama sabasaba mwaka huu 2024.
Bole amesema kuwa sehemu Moja wapo ya uwekezaji ni uwekezaji kwenye Viwanda vya kuzalisha Mbolea nchini kwani Wizara ya Kilimo imejipambanua katika kuhakikisha inaongeza mahitaji ya Mbolea nchini ili kuwa kitovu cha uzalishaji.
“Mamlaka imekuwa ikitumia jukwaa hili la kimataifa kwa ajili ya kuwasiliana na wadau wake kuhusu shughuli zinazofanywa na mamlaka lakini pia inatumia kuhamasisha uwekezaji kwenye biashara na uzalishaji wa mbolea nchini”amesema Bole
Kwa upande wake Afisa biashara na Kaimu Meneja uzalishaji wa ndani na Mazingira TFRA Getrude Ng’weshemi amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu inalenga kuhamasisha wawekezaji wa ndani ambayo inakwenda sambamba na Mamlaka hiyo kuhamasisha wawekezaji.
Aidha Ng’weshemi amesema kuwa hiyo inakwenda sambamba na ajenda ya 10/30 ambayo malengo yake ni kuhakikisha nchi imeongeza uzalishaji wa Mbolea na kupunguza uingizaji wa mbolea kutoka nje ya nchi ifikiapo mwaka 2030
Naye Meneja Maabara kutoka TFRA Leila Robin ameelezea umuhimu wa upimaji wa Mbolea,Maji,Majani na Udongo kuwa ni ili kujua viwango vya urutubisho katika sampuli husika ili kumsaidia mkulima aweze kufanya maamuzi sahihi.
‘Ni muhimu sana ukapima hivi vitu ili ujue viwango vya virutubisho ndani ya sampuli husika ili ukishajua vitakusaidia kuwa na usahihi hasa katika matumizi ya Mbolea”amesema Robin
Matilda Kasanga ni Meneja Uhusiano na Elimu kwa umma TFRA ameendelea kuelezea malengo ya msingi ya TFRA kushiriki katika Maonyesho kuwa wanatumia jukwaa hilo kwa ajili kupata fusa ya kuelezea mchango wa tasnia ya mbolea kwa imekuwa na mchango mkubwa katika kilimo.
‘Pia Jukwaa hili litatupa fursa ya kukuza mahusiano yetu sisi kama Mamlaka pamoja na wadau wetu ambapo tutakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja ambapo ukaribu huu utatusaidia kujenga uhusiano mzuri kwa sisi wadhibiti’amesema Matilda
Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama sabasaba mwaka huu 2024 yanakwenda sambamba na kauli mbiu isemayo ‘Tanzania ni mahali sahihi pa biashara na uwekezaj’hivyo Mamlaka hiyo imewasisitiza watanzania kushiriki ili kujionea uwekezaji ulifanywa kwenye tasnia ya Mbolea.