Meya wa jiji la Arusha, Maxmillian Iraghe akizungumza katika uzinduzi huo mkoani Arusha
Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Consolata Mushi akizungumza katika uzinduzi huo mkoani Arusha.
Meya wa jiji la Arusha ,Maxmilian Iraghe akikata utepe ishara ya uzinduzi huo mkoani Arusha .
………..
Happy Lazaro, Arusha
Meya wa jiji la Arusha Maxmillian Iraghe amezindua msimu wa pili wa mbio za masafa za kiswahili katika viwanja vya Makumbusho ya Azimio la Arusha jijini Arusha zinazotarajiwa kufanyika juni 29 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi Iranghe amesema kiswahili ni lugha kubwa na mbio hizo zinaishi mawazo ya viongozi wa Afrika kama baba wa taifa Hayati Julius Nyerere na Kwame Nkrumah wa Ghana waliokua na ndoto ya kuona Afrika inazungumza lugha moja.
Amesema kuwa jiji la Arusha linaunga mkono mbio hizo na kulipongeza Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa kuasisi mbio hizo na kusema wamefanya jambo kubwa kwa kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kutangaza utalii nchini.
Aidha ametoa wito kwa wafanyakazi wa umma na binafsi na wakazi wote wa Arusha kushiriki katika mbio hizo kukienzi Kiswahili kutangaza utalii wa Arusha bila kusahau kuwa mbio hizo ni sehemu ya kuimarisha afya dhidi ya magonjwa yasiyoambukizwa.
Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Consolata Mushi amemshukuru Mstahiki Meya na Uongozi wa mkoa wa Arusha na wananchi kwa mapokezi makubwa ya Mbio hizo na kutoa wito kwa wadau kuendelea kujisajili kwa ajili ya mbio za Masafa za Kiswahili 2024.
Msimu wa pili wa Mbio za Masafa za Kiswahili 2024 zitakazofanyika kesho mkoani Arusha zitahusisha mbio za kilomita mbili na nusu kwa watoto, na kilomita tano, kumi na ishirini na moja kwa watu wazima pamoja na mbio za baiskeli kilomita hamsini