Na Sophia Kingimali.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi cha Furahika David Msuya ameishukuru Serikali ya Chama Cha Mapinduzi CCM pamoja na wadau wengine wa maendeleo wakiwemo SOS Kwa kuendelea kupeleka wanafunzi kusoma katika chuo hiko huku akitoa rai kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kujifunza katika chuo hiko kwani dirisha la usahili bado lipo wazi na linatarajiwa kufungwa 5 julai 2024.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 28,2024 jijini Dar es salaam wakati akizungumzia mambo mbalimbali ya kijamii Dkt Msuya amesema familia azipaswi kukaa na vijana nyumbani kuna kunaweza kuzalisha vijana wasio na ajira na kupelekea kuingia kwenye makundi ya kihalifu.
“Hapa Chuoni tunazo kozi mbalimbali za ufundi ikowemo udereva,ushonaji,bandari,umeme na kozi nyingine nyingi za ufundi stadi hivyo wazazi wasikae na vijana nyumbani wawalete hapa ili waje kujifunza wakitoka hapa waweze kujiajili au kuajiliwa”,Amesema Msuya.
Akizungumzia ukatili Dkt.Msuya amesema serikali inapaswa kuwashughulikia vikali wanaohusika na maswala ya ukatili lakini kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu ya ukatili kwa jamii hasa kwa kuwafikia wananchi walio vijijini.
Amesema elimu ya ukatili isiishie kutolewa kwa vyombo vya habari pekee kwani kuna ambao wapo pembezoni na hawawezi kuona wala kusikiliza vyombo vya habari na ndio wahanga wakubwa wa ukatili huo.
“Mimi niiombe seriakali kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii kuanzia ngazi ya mtaa/vijiji kwani ndio wanaotendewa zaidi ukatili wapo watu wanaweza kwenda kutoa elimu huko vijijini kama serikali itawawezesha”,Amesema Dkt Msuya.
Sambamba na hayo Dkt Msuya ameiomba Tume huru ya uchaguzi INEC katika utoaji wake wa elimu kuhusu daftari na elimu kuelekea uchaguzi wahakikishe wanawafikia walimu kwa wingi wao kwani wao wakielewa watasaidia kuwaelimisha wengine ikiwemo wanafunzi wao kwani ndio wapiga kura wenyewe.
Sambamba na hayo ametoa rai kwa wananchi kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa na uchaguzi mkuu kujiepusha na vitendo vya rushwa.