Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule akishirikina na Kampuni ya Taifa Gesi kugawa Mitungi 300 ambayo ni sawa na milioni 22 kwa baadhi ya Wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wapili wa Vyuo Vikuu jijini Dar ea Salaam pamoja na Wananchi wa Changanyikeni.
Akizungumza wakati wa Kugawa mitungi hiyo Juni 26, 2024 jijini Dar es Salaam Mtambule amesema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi hayana mkubwa wala mdogo ambaye hatakumbwa na mabadiliko hayo ambayo yanasaabishwa na ukataji wa miti ovyo.
Amesema kuwa hatunauwezo mkubwa wakaupamba namabadiliko ya tabia ya Nchi yanayotokea kwa sura mbalimbali hivyo tupambane na kupunguza mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kutumia nishati safi ili mazingira yabaki Salama.
“Tumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha mazingira yanatunzwa, kuhakikisha mtumizi ya mkaa ambayo yamekuwa kichocheo kikubwa cha uharibifu wa mazingira tunapunguza kwa kiasi kikubwa.” Amesema Mtambule.
Amesem Kampuni ya Taifa gesi inaendeleza nia njema aliyokuwa nayo Rais ya kuongeza kaya zinazotumia nishati safi kupikia.
Akizungumzia kuhusiana na afya za watu Mtambule amesema ili kupunguza mradhi na vifo vinavyotokana na nishati chafu zinazo haribu Mazingira vinatakiwa kitokomezwa kwa nguvu zote kwa kila mwananchi ili kukuza uchumi.
Amesema Matumizi ya Kuni na Mkaa yanamadhara makubwa kwasababu ukiugua matibabu yake ni gharama kubwa na inadhoofisha afya na huwezi kufanya kazi nyingine ambapo mtu akiwa mzima anafanya kazi kujiinua kiuchumi binfsi na uchumi wa taifa nzima.
“Ni mhimu kwa sasa kuongeza idadi kubwa ya wananchi wanaotumia nishati safi na salama ya kupikia.”