Na Sophia Kingimali.
Naibu waziri mkuu na Waziri wa Nishati Dotto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano kubwa la tatu la kitaaluma lenye lengo la kujenga uelewa kwa jamii kuhusu faida ya sekta ya Bahari.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 27,2024 mkuu wa chuo cha bahari DMI Tumaini Gurumo amesema kongamano hilo limatarajiwa kujumuisha nchi 11 za Afrika.
“Hili ni kongamano la tatu na litafanyika Julai 4 na 5 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius nyerere JNICC la kwanza lilifanyika 2022,la pili 2023”,Amesema Gurumo.
Sambamba na hayo Gurumo ametoa wito kwa wataalamu wote wa sekta ya bahari,utalii,bandari,mafuta na gesi,uvuvi na wadau wote wa uchumi wa buluu kutoa ndani ya nchi na nje kujitokeza kwenye kongamano hilo ili waweze kubadilishana mawazo na uzoefu ili kuboresha sekta hiyo.
Akitaja nchi zinazotarajia kushiriki amesema ni Kenya,Komoro,Liberia,Ghana,Nigeria,Sieraleone,Denmark,Italy,Sweeden,Korea kusini na China.
Aidha ameongeza kuwa kongamano hilo limeandaliwa na chuo cha bahari Dar es salaam DMI kwa kushirikiana na chuo cha bahari cha Ghana ambapo mwaka huu linaenda na kauli mbiu isemayo ‘Kuiendea kesho:Kujumuisha Ulinzi na usalama Majini,mabadiliko ya tabia nchi na maendeleo ya teknolojia kwa ukuaji wa uchumi wa buluu’.