Na SHEHA SHEHA, MAELEZO-27/06/2024 |
Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Sleiman Abdulla Salim amevitaka vyombo vya habari Nchini kufanya kazi kwa kuzingatia wajibu wao hasa katika kipindi cha uchaguzi ili kudumisha Amani iliyopo Nchini.
Akizungumza katika Mkutano wa Wadau hao kuhusu wajibu wa Vyombo vya habari katika kuzingatia Maudhui ya utangazaji na muongozo wa kuripoti habari wakati wa Uchaguzi, amesema Vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika hicho hivyo ipo haja ya kufuata maadaili , sheria na kanuni za taaluma yao ili kuepusha uvunjifu wa amani.
mbali na hayo amesema vyombo vyote vya habari vinapaswa kusajiliwa kisheria na kuwataka wamiliki wanaotoa maudhui ya habari mtandaoni kuvisajili vyombo hivyo.
Naye Afisa Sheria wa Tume ya Utangazaji Khadija Mabrouk Hassan amewataka Wanahabari kuacha mihemko, upendeleo na uchochezi ili kuepusha uvunjiffu wa Amani.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Melezo Asha Juma Khamis amesema ni kosa kwa mwandishi wa habari kufanya kazi ya habari bila ya Kitambulisho cha uandishi wa habari kwa mujibu wa Sheria namba 5 ya Mwaka 1988 ya usajili wa Magazeti, Vijarida, Vitabu na uwakala wa habari kifungu namba 39 (1), (2).
Hivyo amewataka waandishi hao kufika Idara ya habari maelezo kwaajili ya kujisajili na kupatiwa Vitambulisho hivyo vitakavyowapelekea kufanya kazi zao kiufanisi na kwa mujibu wa sharia.
Mkutano huo wa Siku mbili umehudhuriwa na wamiliki, wahariri na waandishi mbali mbali katika kujadili kuhusu wajibu wa Vyombo vya habari katika kuzingatia Maudhui ya utangazaji na muongozo wa kuripoti habari wakati wa Uchaguzi.