*Muitikio wa wananchi kupata huduma wazidi kuongezeka
Ikiwa ni siku tatu ya muendelezo wa kambi ya madaktari bingwa na wabobezi mkoani Arusha, watu wengi wamejitokeza kwa wingi katika ushiriki wa kambi hiyo kwaajili ya kupima afya zao na kupatiwa matibabu hali iliyopelekea kuwepo kwa changamoto ya muda kwakuwa wenye uhitaji wamekuwa wengi zaidi.
Kulingana na hilo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda , amezungumza na maelfu ya wananchi waliofika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid na kuwaomba kuendelea kuwa wavumilivu kwakuwa safari ya matibabu si nyepesi na inahitaji utaalamu utakaomshirikisha na Mwenyezi Mungu.
“Poleni kwa safari ndefu, jua kali na kila aina ya changamoto mnayoipata, naelewa ya kwamba kila aliyopo hapa hakutarajia kupata usumbufu aliamini akifika atatibiwa kwa haraka na kuondoka, kutokana na wingi wa watu na muitikio mzuri hivyo changamoto lazima iwe sehemu ya maisha yetu na ombi langi ni kuendelea juwa wavumilivu safari ya matibabu sio nyepesi ili tufike kwenye shauku tuliyonayo”
“Tuwe wavumilivu sababu kwenye matibabu ni eneo muhimu sana la kuwa msikivu na linahitaji utaalamu unaotegemeana na maombi kwa Mwenyezi Mungu tukifanya haraka tunaweza kupewa dawa na kupimwa kipimo si cha ugonjwa wako unaokusumbua na mwishowe tukapata madhara badala ya kupona”
“Nawaomba muwe wavumilivu na muwasikilise madaktari na mfuate maelekezo yao , tufaute utaratb na kusikiliza kwa makini maelekezo yao tusiwe na haraka”