*Awataka kuzingatia maagizo na maelekezo ya ofisi ya CAG
*Apongeza kwa kufunga hoja 62% ataka kumalizia kufunga hoja 38% zilizobaki
-Afurahishwa na mwenendo wa ukusanyaji kodi kwa Halmashauri ya jiji ambapo hadi sasa ukusanyaji ni zaidi ya 108%
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Juni 25,2024 ameshiriki mkutano wa baraza la madiwani la Jiji la hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Serikali (CAG) za mwaka 2022/2023.katika ukumbi wa Arnatoglo Mnazimmoja.
RC Chalamila akiongea katika baraza hilo ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kuwa na historia ya kupata hati safi kwa kipindi cha miaka 8 mfululizo ambapo amewataka kuendeleza utamaduni huo na namna pekee ya kuendeleza utamaduni huo ni kuzingatia maagizo na maelekezo ya CAG pamoja na kuzingatia ushauri unatolewa na wakaguzi wa ndani (Inernal Auditors)
Aidha RC Chalamila amepongeza umahiri wa Halmashauri ya Jiji katika ufungaji wa hoja za CAG ambapo takribani 62% ya hoja zimefungwa hivyo amewataka kuhakikisha wanamalizia kufunga hoja chache zilizobakia.
Sambamba na hilo RC Chalamila ameridhishwa na kufurahishwa na kasi ya ukusanyaji kodi katika jiji hilo ambapo hadi sasa makusanyo yako zaidi ya 108% rai yake kwa Halmashauri hiyo kujipanga zaidi kubuni na kusimamia vema vyanzo vya mapato lakini pia kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kama vile vituo vya kisasa vya Afya na masoko kwa kutumia fedha za ndani.
Vilevile baraza hilo lilihudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt Toba Nguvila, viongozi wa chama,wataalam kutoka ofisi ya mkoa na wataalam wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
Mwisho Mstahiki Meya wa Jiji hilo Mhe Omary Kumbilamoto amemshukuru Mhe mkuu wa Mkoa kwa nasaa zake na kuahidi kwa niaba ya waheshimiwa madiwani kufanyia kazi maagizo yake kwa masilahi mapana ya wana Ilala, Mkoa na Taifa kwa Ujumla