*Wajadili Mradi wa Maboresho Sekta ya Nishati (Energy Sector Reform Programme)
*Serikali yaeleza ilivyotimiza masharti ya EU ili kupata fedha za Maboresho ya Sekta ya Nishati
Dar es salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba leo 26 Juni, 2024, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya (EU) wakiongozwa na Cedric Merel, Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya ambapo mazungumzo yao yalijikita katika kujadili utekelezaji wa Programu ya Maboresho ya Sekta ya Nishati (Energy Sector Reform Programme) inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya.
katika kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Viongozi na Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Fedha, EWURA, TANESCO, NBS na REA. Ambapo EU waliwasilisha vigezo vilvyokubaliwa katika kukidhi masharti ya kupatiwa fedha za utekelezaji wa kazi zilizopangwa.
EU imeeleza kuwa vigezo hivyo vinahusisha kufanyiika kwa mijadala inayohusu sekta ya nishati, kuundwa kwa timu ya Wizara ya ufuatliaji wa miradi na kufanya tathmini, kupunguza upotevu wa umeme na kuendelea kuunganisha wateja wa umeme.
Serikali kwa upande wake imewasilisha hatua zilizofikiwa katika kutimiza masharti hayo kwa mwaka wa Fedha 2023/24 ambapo EU watayapitia na kuyajadili ambapo inategemewa kuwa fedha hizo zitapatikana mwisho wa mwaka wa fedha 2023/24.