Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda akizungumza na wananchi waliofika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa mbalimbali katika kambi ya matibabu ya siku saba inayofanyika bila malipo yoyote yale. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye taasisi yake inashiriki katika kambi hiyo kwa kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi taarifa ya upimaji wa moyo aliomfanyia Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Arusha Shabaan bin Juma wakati wa kambi maalumu ya matibabu ya siku saba ya magonjwa mbalimbali inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na madaktari wa KilMed Air ambao wanatoa huduma ya matibabu ya dharura katika maeneo yasiyofikika kirahisi ikiwemo kwa watalii wanaopata changamoto za kiafya wakati wanapanda mlima Kilimanjaro na wanapotembelea hifadhi za taifa kanda ya Kaskazini. Dkt. Kisenge alikutana na madaktari hao wakati wa kambi maalumu ya matibabu ya siku saba ya magonjwa mbalimbali inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha. Picha na JKCI