Juni 20, 2024 TAKUKURU (W) Itilima Mkoa wa Simiyu, imewafikisha mahakamani Bw. SHEGA NGEME SANGALALI (Mtendaji wa Kijiji cha LUNG’WA), ROMANO PAUL MGANDA (Mtendaji wa Kijiji cha Budalabujiga) na JACKSON NYASILU MBOJE (Mtendaji wa Kijiji cha Mhunze) kwa makosa ya ubadhirifu, ufujaji na matumizi mabaya ya mamlaka kinyume na kifungu cha 28 na 31 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 marejeo ya mwaka 2022 vikisomwa pamoja na aya ya 21 ya jedwali la kwanza na kifungu cha 57(1) na 60 (2) vya Sheria ya Uhujumu uchumi (EOCA) Sura 200 marejeo ya Mwaka 2022.
Kosa la pili ni kutokutii wajibu wa kisheria kinyume na kifungu cha 123 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura 16 marejeo ya Mwaka 2022.
Hatua hii imefikiwa baada ya WATENDAJI hao kwa nyakati tofauti kukusanya fedha za HALMASHAURI (W) Itilima kiasi Cha sh 1,594,000/- kwa njia ya POS na kushindwa kuzipeleka benki kwa wakati kinyume na Sheria na mikataba waliyosaini.
Washitakiwa hao kila mmoja amefunguliwa kesi ya Uhujumu uchumi Na. 16845/2024 R Vs SHEGA SANGALALISANGALALI, 16846/2024 R Vs ROMANO MGANDA na 16847/2024 R Vs JACKSON MBOJE katika Mahakama ya Wilaya ya Itilima ambapo wote WATATU wamekana mashtaka yao na wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti.
Kesi itakuja tena Julai 18, 2024 kwa ajili kutaja hoja za awali. TAKUKURU Itilima. Juni 20, 2024