Maandalizi ya Mkutano wa Kawaida wa 45 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
yanaendelea jijini Arusha katika kikao ngazi ya Maafisa Waandamizi.
Mkutano huo wa Mawaziri utafanyika tarehe 28 Juni, 2024 na unatanguliwa na vikao vya awali vya maandalizi
ambavyo ni; Kikao cha Maafisa Waandamizi kilichoanza tarehe 22 Juni 2024 na kitahitimishwa leo tarehe 24 Juni, 2024 na Kikao cha Makatibu Wakuu kitakachofanyika tarehe 25 hadi 27 Juni 2024.
Pamoja na masuala mengine mkutano huo utapitia na kujadili taarifa mbalimbali kama ifuatavyo, taarifa ya utekelezaji wa maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa na baraza hilo kwenye vikao vilivyopita, taarifa kuhusu masuala ya forodha na biashara na taarifa ya miundombinu, sekta za uzalishaji, sekta za jamii na masuala ya kisiasa.
Taarifa nyingine ni, taarifa ya kamati na fedha na rasilimali watu, taarifa ya mkutano wa Makatibu Wakuu
uliofanyika tarehe 17 Mei, 2024 pamoja na taarifa ya kalenda ya matukio ya jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha kuanzia Julai hadi Desemba, 2024.
Mkutano huu unahudhuriwa na nchi zote wanachama ikiwemo, Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania akiwa mwenyeji, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na
Somalia imeshiriki kwa njia ya mtandao.
=============================
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. |
Ujumbe kutoka Jamhuri ya Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ukifuatilia majadiliano. |
Ujumbe kutoka Jamhuri ya Kenya. |
Ujumbe kutoka Jamhuri ya Rwanda. |
Ujumbe kutoka Jamhuri ya Burundi. |
Ujumbe kutoka Jamhuri ya Uganda. |