Na Ahmed Mahmoud
Serikali imesisitiza kuwekeza nguvu zaidi kwa wale wote walioathirika na urahibu wa dawa za kulevya kwa kuwapatia huduma stahiki ikiwemo kuwarudisha katika Maisha ya kawaida kuwapatia Elimu ya ujasiriamali sanjari na mikopo.
Aidha kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa kupinga dawa za kulevya nchini inaakisi malengo ya mapambano ya vita dhidi ya dawa za kulevya ili kuikinga Jamii hususani Watoto na vijana wasijihusishe na matumizi Wala biashara haramu dawa.
Amesema kauli hiyo inatoa ujumbe wa kutia nguvu kuikinga Jamii hususani vijana wasijihusishe na matumizi na uuzwaji wa dawa za kulevya pia wale wote waliothirika na matumizi warahibu tuwekeze kuwapatia matibabu ya urahibu wa dawa za kulevya na Elimu ya kuwarudisha katika Maisha.
Kwa Upande wake Afisa Elimu na Ustawi wa jamii DCEA Kanda kaskazini Sarah Ndaba ameeleza jinsi mamlaka hiyo inavyotekeleza majukumu yake pia katika kutekeleza kauli mbiu ya mwaka huu DCEA Kanda ya kaskazini itaendelea kuratibu shughuli za kudhibiti na kupambana na tatizo la dawa za kulevya katika Mikoa ya kaskazini Tanga Arusha Kilimanjaro na Manyara zikiwemo shughuli za kuelimisha na huduma za ustawi wa jamii pamoja na operesheni dhidi ya wahalifu wote wa dawa za kulevya.
Amesema Tumeamua kushirikiana na kanisa la wasabato sababu Kuna uhusiano Mkubwa kati ya watu kujihusisha na matumizi au biashara haramu ya dawa za kulevya na kukosa Imani ya mungu na malezi ya kidini tunaamini madhehebu yote yanakataza waumini wao kujihusisha na dawa za kulevya ndio maana tukaamua kuunganisha nguvu kwa sababu ya malezi ikiwa dini zote zinapinga vita dawa za kulevya pia tumetoa Elimu kwa makundi ya watu 300,000 kuanzia juni 2023 Hadi Juni 2024.
Nae Mwenyekiti wa SDA Jimbo la kaskazini ameitaka Jamii kumbuka kujali Afya yako kwani Mungu anawakupenda wala usikubali kubomoa Afya yako kwa kufuata vishawishi mbalimbali vinavyoashiria kuharibu Afya yako.
“Jali Afya yako kwa sababu Mungu anawapenda kwa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya tusiharibu Afya zetu kwa kuharibu Afya zetu”
Awali akitoa ushuhuda Mmoja ya aliyekuwa muathirika wa dawa hizo fredrick Remmy amesema hapo Awali hatukuwa na Elimu ya dawa za kulevya ndio maana wengi wetu tulifuata kampani ila kwa Sasa nimekuwa Balozi naenda kutoa elimu kwa wenzangu ila nilipoteza Mali za familia Nyumba ya Mamaangu mzazi nashukuru Kliniki ya Mkuu wa Mkoa inaendelea kunisaidia kupata haki hiyo hivyo nawahusia vijana wenzangu ogopa sana dawa matumizi ya dawa za kulevya.