Mkurugenzi wa Huduma za Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi ,Kazi,Vijana Ajira na wenye Ulemavu Joseph Nganga akiwakabidhi cheti wahitimu wa program ya mafunzo ya kozi fupi ya uanagenzi baada ya kuhitimu mafunzo hayo katika hafla ambayo imefanyika leo kwenye Ukumbi ulipo kwenye Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Kampas ya bustani jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi ,Kazi,Vijana Ajira na wenye Ulemavu Joseph Nganga (wa tatu katikati) akipiga makofi kufurahia wasilisho la mhitimu wa program ya mafunzo ya kozi fupi ya uanagenzi katika hafla ambayo imefanyika leo kwenye Ukumbi ulipo kwenye Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Kampas ya bustani jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wahitimu wa Program ya mafunzo ya kozi fupi ya uanagenzi na wadau mbalimbali ambao wameshiriki katika hafla ya kukabidhiwa vyeti kwa baada ya kuhitimu mafunzo yao.
………………….
NA MUSSA KHALID,
Serikali imesema itaendelea kutoa program ya mafunzo ya kozi fupi ya uanagenzi ili kuweza kuwa na rasilimali watu toshelevu kwa ubora ili kukuza sekta ya utalii ndani na nje ya nchi.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Huduma za Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi ,Kazi,Vijana Ajira na wenye Ulemavu Joseph Nganga wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vyeti kwa wanafunzi wa kozi fupi ya uanagenzi zaidi ya 233 iliyodhaminiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Nganga amewasihi wanafunzi waliohitimu kozi fupi ya uanagenzi katika Chuo cha Taifa cha Utalii kuhakikisha wanakuwa na ueledi,uadilifu na ubunifu katika mtazamo chanya kwenye kazi ili waweze kufanikiwa zaidi.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema kuwa vijana hao wanakwende kwenye soko la Ajira wakiwa tayari na ujuzi na mafunzo yatakayowawezesha wao kuajirika na kuajirika katika kutoa huduma zinazohitajika katika sekta ya utalii.
‘Rasilimali watu kwenye sekta hii ya utalii ambayo ni muhimu katika kukuza uchumi wetu nimewaasa vijana hawa ili waweze kuwa na ujuzi waliojifunza sambamba na kuwa na mtizamo chanya na kazi jambo litakalowasaidia kuimarika zaidi katika shughuli zao’amesema Nganga
Mkurugenzi huyo amesema kuwa mafunzo hayo yanatolewa katika sekta mbalimbali hasa ya utalii imekuwa ni kipaumbele kutokana na kuwa ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi.
Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Chuo hicho, Dk Florian George amesema mafunzo hayo yalianza mwaka 2013 ambapo hadi mwaka 2022 jumla ya wanafunzi 483 wamehitimu wakiwa na ujuzi wa kujiajiri na kuajiriwa.
Dk George, baada ya ufadhili wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu wanafunzi 150 walidahiliwa.
Ameeleza wanafunzi hao walianza masomo Mei, 2023 na wamehitimu mwaka huu katika kozi za mapishi, mapokezi, uhudumu wa chakula na vinywaji, udobi na uokaji.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi ambao wamehitimu mafunzo hayo katika Chuo hicho akiwemo Evenlight Nyamwanga pamoja na John Shirima wameishukuru serikali kwa kuwezesha mafunzo hayo kwani yamewasaidia kunufaika na ujuzi utakao wasaidia wakati wakiwa kazini.
Wamesema wao kama vijana baada ya kusoma Darasani kwa miezi sita sambamba na kwenda kufanya elimu kwa vitendo yamewasaidia kujipatia nafasi katika maeneo hayo hivyo wamewashauri vijana kutokaa nyumbani bali watumie fursa pindi zinapojitokeza.
Katika hafla hiyo wamehudhuria wadau mbalimbali wakiwemo wasimamizi na mameneja wa hotel mbalimbaliu ambazozimekuwa zikiwapa kipaumbele wanafunzi hao katika ufanyaji wa kazi.