Mufindi, Iringa
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff amemtaka Mkandarasi China Henan International Cooperation (CHICO) kupitia mradi wa RISE kuongeza kasi ujenzi wa barabara ya Mtili-Ifwagi Km 11 na Wenda-Mgama Km 14 zinazojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Iringa.
Ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa barabara hizo wilayani Mufindi na Iringa tarehe 20 Juni, 2024.
Mhandisi Seff amemtaka Mkandarasi CHICO kufanya kazi usiku na mchana ili kufikia lengo kwa mujibu wa mpango kazi na kumaliza kazi kwa muda uliopangwa kwenye mkataba.
Mradi wa RISE una lengo la kuboresha barabara zenye fursa za kiuchumi hasa maeneo yenye uzalishaji wa mazao ya kilimo na unatekelezwa katika mikoa ya Iringa, Tanga, Geitan a Lindi.