Na Mwandishi wetu, Kiteto
WILAYA ya Kiteto mkoani Manyara, imepokea shilingi 949,200,000 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mbunge wa Jimbo la Kiteto Wakili msomi Mhe Edward Ole Lekaita Kisau amedhibitisha kupokewa kwa fedha hizo.
“Ndugu wananchi wenzangu wa Jimbo la Kiteto, nachukua fursa hii kuwafahamisha kuwa tumepokea fedha shilingi 949,200,000 kwa ajili ya miradi ya maendeleo,” amesema Mhe Ole Lekaita.
“Nimezungumza na Waziri wa Tamisemi, Mhe Mohamed Mchengerwa na amethibitisha kuwa pesa zimetumwa na Mkurugenzi wetu CPA Hawa Hassan Abdul amenithibitishia kupokelewa kwa fedha hizo na kuwa fedha hizo zitatumwa katika maeneo husika bila kuchelewa,” amesema Mhe Ole Lekaita.
Ametaja mchanganuo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo, ujenzi wa shule ya msingi mpya ya Olmugi, Kata Namelock shilingi 350,500,000 ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu 6 ya Vyoo shule za msingi Orgira, Kata ya Sunya shilingi 63,600,000.
“Ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu 6 ya vyoo shule za msingi Malimogo, Kata ya Lengatei shilingi 63,600,000 ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu 6 ya vyoo shule ya msingi Enguserosidan, Kata ya Laiseri shilingi 63,600,000,” amesema Mhe Ole Lekaita.
Amesema ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu 6 ya vyoo shule ya msingi Nalangitomon, Kata ya Partimbo shilingi 63,600,000.
Amesema ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa, matundu 6 ya vyoo na madarasa na vyoo ya mfano ya awali shule ya msingi Kurash, Kata ya Lengatei shilingi 157,700,000.
Amesema ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu 6 ya vyoo shule ya msingi Enguserosidan, Kata ya Laiseri shilingi 63,600,000.
“Ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa na matundu 6 ya vyoo shule za msingi Orkitikiti (Engangongare), Kata ya Lengatei shilingi 88,600,000,” amesema.
Amesema ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya sekondari ya Ndirigish Kata ya Ndirigish shilingi 98,000,000.
“Kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Kiteto, tunamshukuru sana
Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote Serikalini,” amesema Mhe Ole Lekaita.
“Tunamshukuru Mhe Rais wetu Mama Samia kwa kuendelea kuboresha maisha yetu wana Kiteto kwa kuendelea kutuletea miradi mikubwa ya maendeleo na kushughulikia changamoto za wananchi katika wilaya yetu,” amesema Mhe Ole Lekaita.
Amesema ahadi za CCM zinaendelea kutekelezwa na wananchi wenzake wa Kiteto, wanayo kila sababu ya kutoa shukrani kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.
“Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan tunamshukuru kwa kuendelea kutupa fedha nyingi kwa ajili ya kutatua miradi ya maendeleo, tumuombee Mhe. Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan Mwenyezi Mungu ampe afya njema na kumlinda vyema ili aendelee na maono yake mazuri katika kujenga taifa letu,” amesema Mhe Ole Lekaita.
“Mhe. Rais wetu mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kusikia kilio chetu kupitia sauti yenu Bungeni, ndugu wananchi wenzangu, kwa dhati kabisa nawahakikishia kuwa nitaendelea kuwa sauti yenu Bungeni na kuwawakilisha ipasavyo kwa unyenyekevu na uaminifu mkubwa,” amesema Mhe Ole Lekaita.
Ametoa wito kwa watumishi wote kuhakikisha kuwa miradi hiyo inasimamiwa vizuri na kwa ufanisi mkubwa ili wananchi wapate huduma hizo kwa wakati.
“Kiteto yetu inaendelea kung’ara! Mungu Ibariki Kiteto Mungu Ibariki Tanzania!, Mungu ambariki Mhe. Rais wetu mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan,” amesema Mhe Ole Lekaita.