………………….
KATIKA kuhakikisha Sekta ya Maji Nchini inaendelea kuimarika, Chuo cha Maji kimeendelea kujiimarisha kuzalisha wataalamu wenye weledi na ujuzi mkubwa unaotakiwa ili kuachana na kutumia au kutegemea wataalamu kutoka nje ya nchi ili kutimiza maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama ndoo
Ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo cha Maji Dkt. Adam O. Karia wakati akielezea umuhimu wa kozi mpya za Uzamili ambazo zitawapa fursa wanafunzi ya kupata ujuzi na maarifa yatakayowawezesha kuchangia kikamilifu maendeleo ya nchi katika nyanja mbalimbali za Uhandisi wa Maji, Usimamizi Rasilimali za Maji na Sayansi ya Mazingira.
Aidha, Dkt. Karia amesema kuwepo kwa program hizo zinatoa fursa na kusaidia kuongeza wataalamu wa kutosha katika Wizara ya Maji na Nchi kwa ujumla pia itawasaidia wahitimu kujiajiri au kuajiriwa sehemu tofauti tofauti ikiwa ni ndani na nje ya Nchi.