Wakulima wa pamba Mkoani Morogoro wamesisitizwa kuzingatia kanuni za upandaji wa pamba ambazo ni sentimita 60 mstari hadi mstari na sentimita 30 kutoka shimo hadi shimo ili kuongeza mavuno na kipato.
Wito huo umetolewa na watafiti kutoka kituo cha Utafiti cha TARI Ukiriguru walipotembelea Wilaya za Ulanga na Mvomero kwa lengo la kukagua maendeleo ya mashamba ya mfano yanayotumiwa kufundishia Teknolojia za kilimo cha zao hilo.
Mratibu wa zao la pamba kitaifa na Mkurugenzi wa Kituo cha TARI Ukiriguru Dkt Paul Saidia, amesema upandaji huo unaongeza idadi ya mimea shambani kufikia 44,444 kwa ekari tofauti na hatua za zamani za sentimita 90 kwa sentimita 30 ambazo hupatikana mimea isiyozidi 15,000.
“katika upandaji huu mkulima anaweza kuvuna kuanzia kilo 1,400 na kuendelea kwa ekari moja” amesema Dkt. Saidia ambaye pia ni mratibu wa mradi wa Cotton Victoria.
Pamoja na upandaji Dkt. Saidia amebainisha hatua za utunzaji shamba ambapo siku ya 70 baada ya kupanda mkulima atatakiwa kukatia ncha za matawi ya shina mama (manual trimming) na kisha siku ya 90 hadi ya 100 mkulima atafanya hivyo hivyo kwenye ncha za matawi yaliyoongezeka ili kusaidia mmea kulea vizuri maua na vitumba.
Kwa upande wake mtafiti kwenye mradi wa Cotton Victoria Dkt Abdullah Mkiga ambaye pia ni Kaimu mratibu wa idara ya uhaulishaji wa teknolojia na mashirikiano amesema kwakuwa upandaji huu mpya unaongeza idadi ya mimea shambani, kasi ya kutembea wakati wa kunyunyizia viuadudu inapungua. Hivyo, mkulima anashauriwa kuwa makini wakati wa kunyunyizia viuadudu ili kila mmea uweze kupata kiuadudu husika. Pia ni muhimu kuzingatia maelekezo ya uchanganyaji wa dawa ili kuwezesha ufanisi.
Dkt. Mkiga, ambaye pia ni Kaimu mratibu wa idara ya Uhaulishaji wa teknolojia na mashirikiano pia anaeleza umuhimu wa kuzingatia maelekezo ya uchanganyani wa viuatilifu ili kuwezesha uf
Ziara hiyo iliyoanza katika Mkoa wa Singida, Dodoma na kisha kutamatika Morogoro ikiwa pia inalenga kutathimini maeneo ambayo siku ya mkulima shambani itafanyika ili kusambaza zaidi teknolojia za zao la pamba hususani hatua mpya ya upandaji wa zao la hilo.