Adeladius Makwega-MWANZA
Tume ya Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa umma imesema kuwa maadili ya utumishi wa umma yanalithishwa kutoka kwa kiongozi mmoja kwenda kwa watumishi , kutoka kwa mkufunzi kwenda mkurufunzi na pia kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto.
“Kama hali inakuwa tofauti yaani mkubwa akakengeuka/akakiuka maadili hilo litakuwa shida kwa jamii nzima na hatari ya kesho ya jamii yetu.’
Haya yamesemwa katika mafunzo ya maadli ya viongozi/ watumishi wa umma katika mafunzo maalumu yaliyofanyika katika viunga vya Chuo cha Maendeleo ya Mchezo Malya (MCSD) wilayani Kwimba, mkoani Mwanza na ndugu Samwel Omari
“Wewe kama kiongozi kila unalolifanya lazima liwe jema, kama wewe kiongozi hauzingatii maadili, walio chini yako unataka wafanye nini? Jambo hilo linaweza kuibua watumishi waovu na hapa jamii inaweza kukengeuka.”
Afisa huyo kutoka tume ya maadili ya viongozi wa umma ambayo jina lake halisi ni Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma alizitaja sifa za mtumshi mwadilifu wa umma kuwa ni;
“Hujali wengine, huwa na moyo mwema kwa wahitaji,huwa mtu mwadilifu huwa msikivu, huwa ni mwaminifu katika hali zote, hutoa ushirikiano kwa wenzake, huwa na heshima na adabu, huwa mnyenyekevu, huwa na bidii ya kazi, hutenda haki na hana tamaa.”
Wakitoa michango yao katika semina hii mkufunzi Mtweve Kayanda aliomba Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa umma kuwa jirani na jamii.
“Ujirani baina ya taasisi yenu na jamii ninavyoona haupo, mjitahidi iwe jirani na wananchi ili muweze kupata taarifa za haya mambo mnayofanyia kazi, ujirani huo utasaidia pia tuweze kuwakosoa hata katika ufanyaji kazi wenu.”
Mkufunzi Wibert Selivery kwa upande wake alitilia maanani juu yasuala la ushoga na usagaji, huku akiomba jambo hilo lifanyiwe kazi kwa kina maana hali ilivyo kwa sasa ni mbaya.
Akihitiisha mafunzo hayo Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Savera Salvatory alisema mafunzo haya yanaendelea maana utumishi wa umma una mambo mengi lakini mambo yote yatafikiwa. B Salvatory alisema kuwa.
“Hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amelisisitiza suala hilo kwa kila Mtanzania maana Watanzania tuna maadili yetu tangu enzi.”
Mafunzo haya bado yanaendelea huku yakihusisha wataalamu kutoka idara mbalimbali za umma.