Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanal Evans Mtambi amezipongeza Taasisi zinazojihusisha na kulea watoto yatima pamoja na wenye mahitaji Maalum na wale wanaokabiliwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia ambapo amewataka Viongozi wa vituo hivyo kuhakikisha wanasmamia Malezi bora kwa watoto.
Kanal Mtambi ametoa kauli hiyo wakati akipokea na kutoa Mkono wa Eid hadhah kutoka kwa viongozi wa msikiti wa Al-Jazeera wilayani Musoma Mkoani Mara ambapo amewataka Viongozi kuhakiki wanawalea watoto katika maadili mema ili kuhakikisha linakuwa na watoto wenye maadili mema
” Hongeren kuisaidia Serikali katika upande huu hasa wakuwalea watoto wenye uhitaji tunahitaji kuona watoto wanakua katika maadili mema niwaombe Sana mnapopata changamoto msisite kuwasiliana na Sisi kama viongozi wenu tuwasaidie Sisi wote tunaijenga Serikali moja inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan”Alisema Mtambi Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Katika hatua nyingine Mtambi amesema mmomonyoko wa maadili kwa sasa nijanga linalolikumbuka Taifa hivyo kama viongozi wa taasisi wanawajibu Mkubwa wakuisaidia Serikali katika Malezi kwa kiasi kikubwa.
Aidha kwa upande wake meneja WA kituo cha kulelea watoto cha Al-Jazeera Meneno Hamisi ameishukuru Serikali kwanamna ambavyo inavipa nguvu vituo hivyo katika Malezi licha ya changamoto nyingi vinavyovikabili vituo hivyo ambapo ameiomba Serikali kuendelea kunikumbuka kuvisaidia vituo hivyo.