Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Arusha,Frank Mbando akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha
Makamu wa Rais Dkt .Philip Mpango
…………..
Happy Lazaro ,Arusha .
Makamu wa Rais,Dkt Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, maadhimisho ya jubilee ya Miaka 50 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Mashariki, kati na kusini mwa Afrika inayoshughulikia sayansi ya Afya (Eastern, Central and Southern Africa Health Community, (ECSA-HC),yatakayofanyika kesho jijini Arusha.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Arusha,Frank Mbando alibainisha hayo wakati akiongea na waandishi wa habari katika kongamano hilo la sayansi ya Afya linaloendelea jijini hapa.
Amesema katika maadhimisho hayo wananchi zaidi ya 500 watanufaika na huduma ya kupima na kuchunguza afya zao bure ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo , kuchunguza magonjwa yasiyoambukiza kupatiwa tiba.
Amesema taasisi ya ECSA ni munganiko wa nchi wanachama zipatazo 9 na makao Makuu yake yapo jijini Arusha,inaadhimisha miaka 50 tangia kuanzishwa kwake na kilele chake kitafungwa rasmi juni 19 mwaka huu na dkt Mpango.
Mbando amesema pamoja na mijadala ya kisayansi inayoendelea kuhusu tafiti za afya,ECSA iangalie namna ya kujikomboa na kujitegemea zaidi katika sekta ya afya, katika mazingira ya uwezeshaji wa dawa na vifaa tiba ukizingatia kwamba bado nchi za afrika zinategemea zaidi kuagiza vifaa tiba na dawa ambavyo ni gharama kubwa kutoka nje ya nchi zao.
“Juni 19 mwaka huu ndio kilele cha Maadhimisho ya miaka 50 ya jubilee ya ECSA,tunatarajia dkt Mpango kuwa mgeni rasmi na kwamba kabla ya hapo tutashuhudua kambi ya uchunguzi wa matibabu bure ni vizuri wananchi wakatumia fursa hiyo kuangalia afya zao na na huduma hiyo inatolewa bure bila malipo”Alisema Mbando.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Yoswa Dambisya amesema kabla ya kilele cha maadhimisho hayo wataalamu wa afya wapatao 250 wamekutana kutoka mataifa mbalimbali kwa lengo kubadilishana uzoefu na kuwasilisha mafanikio ya tafiti mbalimbali za afya.
Dkt Godfrey Sama ambaye ni mmoja ya waandaaji wa Kongamano hilo amesema kilele cha Maadhimisho hayo kitakwenda sanjari na zoezi la uchangiaji damu na pia wanatarajia kutoa huduma ya uchunguzi wa afya kwa watu zaidi ya 500 Katika kambi iliyopo general tyre Arusha.