Mwanzilishi na mmiliki wa kituo hicho cha Ubora design ,Christopher Lee Plummer akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho,Lucy Plummer akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha
Baadhi wa wageni mbalimbali waliofika katika uzinduzi huo kujionea vifaa mbalimbali vinavyopatikana katika kituo hicho.
…………….
Happy Lazaro, Arusha .
KAMPUNI inayoongoza kwa usanifu na ubunifu ya Ubora Design imezindua kituo kipya cha maonyesho na ubunifu katika hoteli ya Grand Melia Arusha ambapo ni cha kisasa na kinaonyesha kilele cha ufundi wa ndani na ubora wa ubunifu .
Kituo hicho ambacho kimeanzishwa na mbunifu aliyeidhinishwa na LEED ,Christopher Lee Plummer amesema kituo hicho kinaleta viwango vipya vya usanifu endelevu na ubunifu katika eneo hilo la Afrika Mashariki.
Plummer amesema kuwa ,Ubora design inajishughulisha na usanifu wa kipekee ,huku ikitoa huduma kamili katika duka hilo kwa ajili ya usanifu na ujenzi .
Ameongeza kuwa,wanachokifanya wao ni kuhakikisha wateja wanapata usalama na ujasiri wa utekelezaji mzuri wa miradi kutoka kwenye dhana hadi kukamilika,ambapo imekuwa ikitetea maendeleo endelevu na ya kimaadili kwa kuwa yana manufaa makubwa kwa watu wa Tanzania .
“Mimi ni mzaliwa wa Tanzania niliyekulia Dar es Salaam na nilihamia Marekani akiwa na miaka 17 ,na niliendeleza kazi yenye mafanikio makubwa huko New York City,nikifanya kazi kwenye miradi mingi ya hashi ya juu,ambapo miaka kumi na miwili iliyopita niliamua kurudi Tanzania kwa lengo la kubadilisha dhana ya usanifu na ujenzi katika nchi yangu,na tangu kurudi kwangu nimepanua uwepo wa Ubora Design na kufungua ofisi Rwanda na kufanya kazi kwenye miradi mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki.”amesema .Plummer.
Hata hivyo ameahidi kuleta maendeleo kupitia miradi yake ambapo kupitia kituo hicho amekuwa akitoa elimu mbalimbali kwa vijana juu ya usanifu endelevu na matumizi ya vifaa nasikia huku akiwahimiza kukidhi viwango vya kimataifa.
Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho,Lucy Plummer amesema kuwa kituo hicho kipya cha maonyesho na ubunifu ni ushahidi wa kile kinachoweza kufanywa kwa viwango vya juu kwa kutumia rasilimali za ndani kwani hakionyeshi tu njia ya ubunifu na endelevu ya Ubora design bali pia kinahamasisha miradi ya baadaye katika eneo hilo.
Amewataka wananchi pamoja na wadau mbalimbali kukitumia kituo hicho kwa ajili ya kununua bidhaa mbalimbali za asili na zilizobora zaidi kwa matumizi mbalimbali ya hoteli pamoja na matumizi ya nyumbani na kuweza kuendeleza utalii kwa ujumla.
“Tunafurahi kufungua kituo chetu kipya cha maonyesho na ubunifu hapa jijini Arusha ,na nafasi hii inaonyesha maono yetu ya kuchanganya ubunifu wa zamani na kisasa ,na tunafurahi kuonyesha kile kinachoweza kufanywa kwa kutumia rasilimali za ndani,lengo letu likiwa ni kuhamasisha na kuongoza njia ya maendeleo ya kimaadili na endelevu nchini Tanzania na kwingineko.”amesema .
Nao.baadhi ya wadau waliofika katika uzinduzi huo,wamesema uwekezaji uliofanywa na mdau huo ni mkubwa sana na unachochea masuala ya utalii sambamba na kuwezesha watu kupata elimu ya kutosha kuhusu masuala ya ubunifu na namna ya kuweza kuboresha bidhaa zetu ili.ziwe na ubora wa hali ya juu.