Na Sophia Kingimali
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa usajili wa biashara na leseni BRELA Godfrey Nyaisa amesema wataendele kufanyakazi kwa karibu na waandishi wa habari ili kuhakikisha umma unapata taarifa sahihi kutoka kwa BRELA na hatimae kufanya maamuzi ya kusajili Biashara zao na kuzirasimisha.
Hayo ameyasema leo Juni 18, 2024 jijini Morogoro,wakati wa Mafunzo Maalumu ya BRELA kwa Waandishi wa habari wanaoripoti Mkoa wa Dar es Salaam ambapo lengo ni kuwajengea uwezo utakaowezesha waandishi hao kuandika kwa weledi habari za Wakala huo.
“matarajio yetu baada ya mafunzo ni kuwa mabalozi wazuri katika kuhabarisha shughuli mbalimbali matarajio yetu baada ya mafunzo ni kuwa mabalozi wazuri katika kuhabarisha shughuli mbalimbali za BRELA ili kuleta mageuzi katika jamii”,Amesema Nyaisa.
Amesema zipo bunifu na vumbuzi mbalimbali zinafanyika katika jamii ila waandishi wanapoandika masuala ya usajili wa Alama za Biashara na Huduma pamoja na Utoaji wa Hataza jamii itaona, itasikia na itasoma na kupelekea kuona umuhimu wa wao kulinda kazi zao ambazo mwisho wa zitaleta heshima katika taifa letu.
“BRELA ili kuleta mageuzi katika jamii hasa katika bunifu na vumbuzi mbalimbali zinafanyika katika jamii ila nyie mnapoandika masuala ya usajili wa Alama za Biashara na Huduma pamoja na Utoaji wa Hataza jamii itaona, itasikia na itasoma na kupelekea kuona umuhimu wa wao kulinda kazi zao ambazo mwisho wa zitaleta heshima katika taifa letu”,Amesema.
Sambamba na hayo Nyaisa amesema kuwa WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA) wataanza kutoa tuzo Maalum kwa waandishi wa habari za biashara ambao watakuwa wakiandika makala zenye matokeo chanya kwa jamii lakini makala ambazo zitakuwa zimejitosheleza.
“Tutakuwa na tuzo maalum kwa waandishi wa habari ambao watakuwa wanaandika Makala zinazohusu BRELA.Tutakuwa tunashindanisha makala hizo na mshindi wa kwanza ambaye atakuwa ameandika makala Bora atapewa tuzo na itakuwa ENDELEVU,”amesema Nyaisa.