FewMkuu wa Kitengo Cha Afya mkoa wa Arusha Dkt. Omary Chande akizungumza katika mkutano huo unaoendelea mkoani Arusha Lazaro,Arusha .
……….
Wataalamu na Watafiti mbalimbali wa masuala ya Afya kutoka nchi tisa wanachama wa Jumuiya ya afya inayohusisha nchi za Mashariki, kati na Kusini mwa Afrika (ECSA-HC) wamekutana mkoani Arusha kwa lengo la kuwasilisha tafiti za afya walizofanya katika nchi zao na kuweza kujadili kwa pamoja.
Aidha kupitia mkutano huo kwa 14 kwa pamoja wataweza kujadili tafiti hizo zilizofanywa Kuhusiana na shughuli za Afya kwa lengo la kupata majibu sahihi na kuweza kuangalia eneo la kufanya maboresho na kuweza kujifunza kutoka kwa nchi zingine.
Akifungua Mkutano huo Mkuu wa Kitengo Cha Afya mkoa wa Arusha Dkt. Omary Chande amesema mkutano huo ni wa kisayansi na unalenga kupata Majibu kutokana na tafiti za Afya zilizofanyika katika nchi Mbalimbali Kwa lengo la kuijenga Jamii kupata uelewa wa Afya Kwa wote .
Dk.Chande amesema kuwa,baada ya kuwasilishwa kwa.machapisho hayo ya tafiti mbalimbali zilizofanywa na watalaamu hao itasaidia sana katika kuchukua hatua za haraka dhidi ya magonjwa mbalimbali na kuepukana na madhara ambayo yangeweza kutokea .
“Tunashukuru sana( ÈCSA -HC ) kwa kuzikutanisha nchi tisa ambazo ni Tanzania,Kenya,Uganda,Lesotho,Eswatini,Malawi ,Mauritians,Zambia,na Zimbambwe kwa kutuletea mkutano huu hapa kwani utaleta mafanikio makubwa sana katika sekta ya afya hapa nchini kutokana na kubadilishana mawazo na wenzetu kutoka nchi hizo na kuweza kujifunza namna walivyoweza kufanikiwa katika masuala mbalimbali ya afya .”amesema Dk.Chande.
Naye Katibu Tawala msaidizi anayehusika na viwanda ,biashara na uwekezaji mkoa wa Arusha , Frank Mmbando amesema kama nchi za Afrika wanapaswa kujiangalia namna gani wanaweza kujikomboa katika eneo la afya Kwa kuwa na mazingira ya uwezeshaji wa Afrika kijitegemea katika dawa na vifaa Tiba.
Mmbando amesema kuwa,uwasilishaji wa tafiti hizo kutoka nchi hizo utasaidia kwa kiwango kikubwa kuangalia sisi kama.nchi za Afrika namna ya kujikomboa zaidi katika masuala ya afya.
Aidha amesema kuwa,pamoja na utafiti huo wa kisayansi unaofanywa na nchi hizo ni vizuri wakaangalia namna ya kuweza kujitegemea zaidi katika eneo la dawa na vifaa tiba ili kuweza kuwa ba sawa za kutosha.
Naye Dk .Mpoki Ulisubisya kumekuwepo na changamoto ya idadi kubwa ya wananchi kutumia sawa kiholela bila kufanya vipimo hatua ambayo amesema inachangia ugonjwa kuendelea kuwa sugu ,hivyo amewataka wataalamu wa afya kujenga utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi kufanya vipimo kabla ya kutumia dawa.
Dk. Ulisubisya amesema kuwa,changamoto kubwa iliyopo ni utafiti unaofanywa wa kuzalisha dawa za kutibu haujaendana na kasi ya uhitaji uliopo ,ambapo amewataka wananchi kujijengea utaratibu wa kutumia dawa za hospitali kwani ndizi sawa sahihi.
Kwa upande wake Prof. Tigan Moyo kutoka Zimbabwe amesema kuwa,Wizara za Afya kutoka nchi Mbalimbali zimekuwa zikifanya jitihada kuhakikisha sekta ya afya inaimarika hususani Kwa Usalama wa wananchi hivyo mkutano huo unaangazia mchango wa wataalamu hao katika sekta nzima ya afya .
Hata hivyo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kilele Cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya ECSA -HC yatakayofanyika mkoani Arusha juni 19.