Adeladius Makwega-MWANZA
Wakristo wemeambiwa kuwa wanaposali Jumapili ya Juni 16, 2024 wanahimizwa kuyashika maneno ya Mungu, wayaishi maneno ya Mungu maana neno hilo linawatia nguvu, neno hilo hilo linawapatia uponyaji na zaidi ya yote neno hilo hilo linatuimarisha katika ufuasi wetu kwa Mungu.
“Mungu mara zote anakaa katikati yetu ili tupate uimara, ili tupate wokovu, alifanya hivyo kwa taifa lake Israel, anafanya hivyo hata katika nyakati zetu za leo, leo hii anazungumzia habari za ufalme wake akiulinganisha na mbegu iliyapandwa bila kuifuatiliwa na baadaye ikazaa matunda, anafananisha na punje ndogo iliyo ndogo kuliko zote hpa maana yake sisi kama watoto Mungu lazima tukue, lazima tukomae na lazima tuzae matunda mema.”
Padri Samson Masanja ambae ndiye Paroko wa Parokia ya Malya alihubiri hayo katika Kanisa la Bikira Maria, Malikia wa Wamisionari Parokia hii hii ya Malya Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza ndani ya Misa ya Kwanza ya dominika 11 ya mwaka B wa liturijia ya kanisa.
Waamini hao katika mahubiri ya dominika hii waliulizwa maswali haya,
“Tangu tumeipokea imani yetu; Je imani yetu inakuwa ? Je Imani yetu inakomaa? Je imani yetu inazaa matunda mema?
Katika maisha yetu ya kila siku jinsi tunavyotendeana sisi kwa sisi, mbegu hiyo inakuwa, inakomaa na inaiva na kuzaa matunda mema .”
Katika Misa hiyo iliyoanza saa 12.00 ya asubuhi ilipofia saa 12. 38, kabla ya Sala ya Kanuni Imani waliingia nyuki kanisani humo, waamini wakiombwa wawe watulivu.
Kwa utafiti mdogo uliyofanywa na mwandishi wa ripoti hii eneo la Malya na viunga vyake lina nyuki wengi na cha kusikitisha eneo hilo halina mfugaji mkubwa wa nyuki na inaonekana jamii haijapata uhamasishaji mkubwa.Huku bei ya asali ya nyuki wakubwa kwa lita inalingana na bei ya Miji Mikubwa kama ile Dar es Salaam na Arusha nchini
Tanzania.Nyuki hao wengi wakirandaranda katika makazi na kuweka makazi katika majengi ya umma.
Hadi misa hiyo inamalizika majira ya saa 2.00 asubuhi nyuki hao hawakuleta madhara kwa waamini hao katika misa hiyo ya kwanza.