………
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeshiriki maonesho ya Mnada wa Mifumo 2024 kama Mdhamini Mkuu yalioanza Juni 14, 2024 katika Viwanja vya Ubena Zomozi, Chalinze Mkoani Pwani.
Benki ya TADB kudhamini maonesho hayo ni sehemu ya jitihada za benki kuweza kukutana na wafugaji mbalimbali nchini ili kuwaelimisha na kuwaunganisha na fursa za uwekezaji katika sekta ya mifugo hasa katika ufugaji wa kibiashara.
Akizungumza katika maonesho hayo Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)
Bw. Frank Nyabundege amekipongeza Chama cha wafugaji wa ng’ombe Bibiashara (TCCS) kwa kuandaa maonesho ya mifugo na mnada na kuahidi kuwa TADB itaendelea kuwa mdhamini mkuu wa maonesho hayo.
TADB imetoa mkopo wa kiasi cha shilingi bilioni 26 na Ng’ombe wa Maziwa 1,748 katika sekta ndogo ya maziwa na shilingi bilioni 1.871 katika sekta ndogo ya unenepeshaji wa Ng’ombe wa Nyama.